(+video) Muuguzi amchezea densi mtoto aliyelazwa hospitalini

''Tunastahili wahuduma kama hawa'' mwingine aliandika.

Muhtasari

• Muuguzi huyu alimtumbuiza mtoto huyo ambaye angekuwa na upweke kutokana na hali ya amelazwa hospitalini.

Muuguzi  mmoja aligeuka gumzo la siku baada ya kuonekana kwenye kanda ya video akimchangamsha mtoto aliyekuwa mgonjwa kwa ngoma maridadi ikiambatanishwa na densi.

Muuguzi huyo aliyetambuliwa kwa jina  Lukresia Robai alishabikia kwenye mitandao ya kijamii kwa upendo wake aliouonyesha kwa mtoto yule mchanga.

Nesi huyu ambaye pia ni mwanatiktoker alikuwa akimpa tabasabu mtoto yule ambaye angejihisi mpweke kutokana na hali yake ya kulazwa hospitalini.

Mtoto huyo alionekana amejawa na furaha isiyopimika huku akitingiza bega kutokana na mdundo wa ngoma ya "Baby Shark" waliokuwa wakiimbisha.

Densi hiyo iliwafanya watu wengi walioiona kuitazama mara kwa mara nao wengine wakituma msururu wa jumbe ambazo zilionekana kumpongeza muuguzi yule kwa kitendo chake cha huruma na kumpa mtoto furaha sawia na ya mama mzazi.

''Ikiwa unamjua msalimie, asante kwa kuleta furaha kama hii kwa mtoto huyu mdogo. Milango yako katika taaluma hii ifunguke zaidi na zaidi.'' mmoja wa watazamaji alimtakia muunguzi yule mema maishani mwake.

''Tunastahili wahuduma kama hawa'' mwingine aliandika.

''Hii video inanifanya moyo wangu kuwa na furaha'' Cynthia Mwangi alisema.

''Mungu ambariki, Madaktari wengi huwa na hasira kila wakati'' Eldad Makokha alisema.

''Nina furaha ninapoona bidii yake ya kujitolea kazini. Mungu ambariki'' Godfrey Ole Meigurana alisema