Vivianne amtambua Sam West kama 'Murife' huku akikumbuka alipochumbiwa

Sam West alimvisha Vivian pete ya uchumba wakati wa kipindi cha moja kwa moja kwa runinga

Muhtasari

• "Ndiye huyo Murife," Vivianne aliandika huku akipakia video hiyo ya wakati alipovishwa pete ya uchumba.

Vivianne na Sam West
Image: Maktaba

Mwanamuziki Vivianne amepakia picha ya kumbukumbu za aliyekuwa mpenzi wake, Sam West alipomwomba uchumba katika kipindi cha 10/10.

Katika ukurasa wake wa Instagram, Viviane alizungumzia video hiyo na kumbandika Sam West jina la 'Murife'.

Jina hilo linatumika kama jina la majazi kulinganisha mtu anayependa kukimbia au kutoroka panapotokea jambo.

"Ndiye huyo Murife," Vivianne aliandika huku akipakia video hiyo.

"Mwanamke ambaye yuko mbele yenu ni malkia na anahitaji mwanamume ambaye atamjengea ikulu, ni zaidi ya malkia. Vivianne nina jambo ambalo ninataka kukuambia, nina zawadi yako," Same West alisema huku akimvisha Vivianne pete ya uchumba.

Sam West alimvisha Vivian pete ya uchumba wakati wa kipindi cha moja kwa moja kwa runinga, na wawili hao walikuwa wamechumbiana kwa muda.

Hivi majuzi,kwenye Facebook, mwanamuziki huyo alikuwa amedokeza kuwa West alitaka kumrudia baada ya uvumi kuwa walitengana.

Aliwauliza mashabiki wake maoni yao kuhusu jambo hilo.

"Ni nini kingekufanya umrudishe mpenzi wa zamani  baada ya mwaka mmoja au miwili ya kuwa mbali na wewe," aliandika kwa kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Wafuasi wake walitoa maoni tofauti katika majibu yao.

“Anarudi kifedha ama kimapenzi. Kumrudia Ex wako ni kama kufanya harakati ya kujitia kitanzi, huwa haiishi vyema,” Maggie Mwajuma alimwambia.

“Mambo Na ex wachana..hautakua ukiendelea kung'ang'ania yaliyopita..acha yaliyopita yawe yamepita na ushughulikie sasa na yajayo..” Douglas Babu alimshauri.

“Kiburi cha watu wengi ndiyo hutuma waishi kujuta,,,mapenzi hayana mwisho,,,ni ile tu watu wanakataa,,,,kama unampenda mtu,,,usikatae,” mwingine alikuwa na mawazo tofauti.

Vivianne aliibuka na muonekano mpya wa nywele baada ya kutengana na mchumba wake.

Wawili hao walikuwa na familia iliyochanganyika. Wakati Vivian alikuwa na binti, Sam West alikuwa na mtoto wa kiume kutoka kwa uhusiano wa awali.