Mchekeshaji Eric Omondi amefichua kuwa mpenzi wake Lynne alipoteza mimba.
Omondi alifichua haya siku ya Jumanne kupitia Instagram kuwa Lynne alipoteza mimba licha ya jitihada za kujaribu kumwokoa mwanawe.
Watu wengi mashuhuri na mashabiki waliwatumia jumbe za kuwapa pole na kuwafariji kutokana na tukio hilo.
"Pole sana Eric Omondi na Lynne, Mungu awape nguvu kwa wakati huu," eddiebutita alisema.
"Poleni Sana. Mungu awe na nyinyi kwa wakati huu mnaopitia jambo hilo," mpinzani wa Omondi, Bienaimesol aliwafariji wapenzi hao.
"ππππSiwezi kutafakari mnachokipitia, poleni," Nasra Yusuf alisema.
"Poleni sana.Mungu anelewa ni kwa nini mmepitia hiki. Natumai atawapa amani wewe na Lynne," aggie_the_dance_queen alisema.
"Oh my .. poleni Sana broπ₯π₯ππΏππΏππΏ," Namelesskenya aliandika.
Omondi alikuwa amepakia video yake na Lynne wakiwa hospitalini huku mpenzi huyo wake kujiangusha akilia na kushikiliwa.
Aliandika ujumbe akiwafahamisha watu na kwa wakati huo huo akimwandikia mwanawe ujumbe.
"Jana usiku ulikuwa miongoni mwa usiku mrefu maishani mwanguπ₯π₯. Tulijitahidi kwa zaidi ya saa 5 ili kujaribu kumwokoa malaika wetu mdogo ila Mungu alikuwa na mipango mingine. Hatukukutana nawe ila tulikuhisi na kuwa na kumbukumbu zako na tutazidi kukupenda milele πππ―π―. Heshima kwa wanawake wote, hakuna mwanaume duniani mwenye nguvu kama hiyo. @l.y.nn.e kuwa na nguvu.. Yote yatakuwa shwari....," Omondi aliandika.