Amber Ray avalishwa pete ya uchumba na Kennedy Rapudo

Amber Ray amevalishwa pete ya uchumba akiwa kwenye mtoko Dubai

Muhtasari

• Kennedy Rapudo alimwandalia Amber Ray hafla ya kumwomba  uchumba mjini Dubai.

Amber Ray na Kennedy Rapudo

Mwansosholaiti Amber Ray amevishwa pete ya uchumba na mpenzi wake Kennedy Rapudo wakiwa nchini Dubai.

Rapudo alimpeleka Amber nchini Mauritius ili kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kabla ya kumpeleka Dubai ambapo alimposa Amber.

Mchumba huyo wa Amber Ray alimwandalia miadi ya kimahaba iliyokuwa na mishumaa kando ya bahari.

"Usiku unaofaa kukumbukwa," Amber Ray aliandika Instagram huku akipakia video ya hafla tukio hilo.

Katika ukurasa wake wa Instagram, Rapudo alisema kuwa atamfanyia Amber chochote cha kupendeza kama ishara ya upendo wake kwake.

Mashabiki wake waliwapongeza kwa hatua yao na kuwatakia mema.

"Hongera ❤️❤️unastahili furaha yote,"anita sonia alisema.

"Napenda ❤️ Hadithi hii yenu ya mapenzi 😍Hongera 🎉,"yvonneafrostreet aliandika.

"Mwanaume mzuri huja na uwazi mwingi na amani nyingi❤️❤️🔥🔥😍😍unastahili haya yote,"ahasha yanoh alisema.

Sikulala nilikuwa nikingojea hii! Nina machozi ya furaha. NIMEFURAHIA ,AMBER HONGERA,"___shan0 alisema,.

Wow. Endelea kutufurahisha. Msiwahi jaribu kuachana nyinyi maanake tunapenda mapenzi ❤️❤️❤️ hongera sana," rey_blessed aliandika.

Hivi majuzi, wawili hao walikuwa wamedhaniwa kuchumbiana tayari baada ya dada yake Amber kupakia video iliyodhaniwa kuwa sherehe ya kuchumbiana.

Amber Ray alikana madai hayo na kufafanua kuwa walikuwa wanawajulisha wazazi wao kuwa wako kwenye mahusiano.

"Nawashukuru nyote kwa jumbe mlizonitumia ila kama kawaida wanablogu wamewachanganya kidogo. Haikuwa sherehe ya kuchumbiwa, ilikuwa ni kuposa tu  (ili wazazi wetu kufahamu kuwa tuko kwenye mahusiano) , hii ilikuwa hatua kubwa sana kwetu," mwanasosholaiti huyo alisema.