logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mzee aibuka na kudai kuwa baba wa kijana aliyetuzwa kwa kuokoa watu ajali ya ndege TZ

Kwanza mimi nilitoka nyumbani katika hali ya kuenda kutafuta maisha - Mzee huyo alisema.

image
na Radio Jambo

Makala10 November 2022 - 09:15

Muhtasari


• Mzee huyo alisema kwamba alimwacha kijana huyo akiwa na miaka mitatu na kuondoka si kwa kutoroka bali kwa ajili ya kutafuta maisha.

Jackson Majaliwa na mzee anayedai kuwa babake

Mapema wiki hii baada ya ajali mbaya ya ndege ya Precision Air kuanguka kwenye ziwa Victoria. Habari kuu pia ilikuwa kuhusu kijana mmoja kwa jina Jackson Majaliwa ambaye alitambuliwa kama shujaa kwa kitendo chake cha kufanay udhubutu wa kuwaokoa wasafiri waliokuwa ndani ya ndege ile.

Kijana Majaliwa ambaye ni mvuvi alikuwa katika shughuli zake za kila siku kutafuta riziki wakati ndege hiyo ilipoanguka ziwani na akafanya hima ya kuvunja mlango wa ndege na kuwaokoa jumla ya watu 24.

Baadae rais Samia Hassan alitangaza kijana yule kupewa kazi katika jeshi la uokoaji na zimamoto kando na kukabidhiwa zawadi ya shilingi milioni moja za kitanzania.

Sasa baada ya kunukia mafanikio, babake ambaye alisemekana kutoroka familia yake miaka mingi ameibuka na kudai kwamba Majaliwa ni mwanawe na hata kusema ni yeye alimpa jina.

Mzee Jakcson Samwel alizungumza na Ayo TV na kusema kwamba ni mwanawe hata kama alikwepa familia ila si kukwepa kwa ubaya bali ni hali ya kuondoka nyumbani kutafuta maisha.

“Kwanza mimi nilitoka nyumbani katika hali ya kuenda kutafuta maisha. Tulikutana msimu wa kudaka senene na tukampata mtoto Majaliwa japo nilimkuta bado yeye ana familia yake, watoto kama wawili. Lakini kutokana na ugumu wa maisha nikalazimika kuondoka kwenda kutafuta maisha sehemu nyingine. Sisi hatukuachana bali tulitengwa kimaisha, ina maana mimi nilitoka na niliendelea kufanya vile kilichokuwa kinapatikana natuma. Na mpaka dakika hii tuna mahusiano mazuri tu na mamake Majaliwa,” mzee huyo alisema.

Mzee huyo alieleza kuwa kuondoka kwake hakukuwa kwa njia ya shari bali ni umbali tu uliwatenganisha ila kusisitiza kuwa bado wanazidi kusemezana na kusaidiana kwa ajili ya mtoto.

Awali mamake Majaliwa alizunguzma na vyombo vya habari ambapo alisema anafanya biashara ya kuuza mkaa wa rejareja na kusema alimlea kijana huyo peke yake kwani babake alimtoroka mtoto akiwa na miaka 3 tu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved