Willy Paul asema sababu za kuwa na kiburi

"Halafu si niko na pesa na maisha mazuri na mimi ni mwanaume mjaluo mzuri ?

Muhtasari

• Alisema... Zaidi ya hayo mimi ni mwanamuziki ambaye ana talanta zaidi ya wengine hapa Kenya? Baaas".

Willy Paul azungumzia kupitia unyongovu
Willy Paul azungumzia kupitia unyongovu
Image: YouTube screengrab

Mwanamuziki Willy Paul amejibu madai ya wanamitandao kwamba ana kiburi, huku akionekana kutojalishwa na jambo hilo. 

Katika Instastory zake, Pozee aliwaambia mashabiki wake kuwa yuko huru kufanya anachotaka kwani yeye ni mtu mzima.

"Eti niko na kiburi? Waah hilo si jambo zuri lakini si kila mmoja na maisha yake? Si hakuna anayenilisha?" Pozee aliandika.

Alisema kuwa maisha anayoishi yanamruhusu kuwa na kiburi kwa kuwa hakuna anayefahamu vyema maisha yake.

"Halafu si niko na pesa na maisha mazuri na mimi ni mwanaume mjaluo mzuri ? Zaidi ya hayo mimi ni mwanamuziki ambaye ana talanta zaidi ya wengine hapa Kenya? Baaas!" Pozee alisema.

Haya yamejiri siku chache bada ya mwanamuziki huyo kununua gari jipya na amekuwa akijigamba na gari lake ta kujigamba kwa magari yake.

Pozee amekuwa akipakia video akiwa amevaa nguo zilizofanana rangi na gari lake jipya.

Aliyapachika magari yake majina ya majazi, gari la rangi ya manjano likiitwa Rihanna na gari lake la kitambo jeupe likiitwa Beyonce.

"Ilikuwa ngumu kufika nilipo sasa ila namshukuru Mungu. Kwa sasa nimewapa watoto wangu majina. Magari yangu yote ambayo ni ghali mno yana majina sasa. Mzizoee sawa?" Mwanamuziki huyo alisema.

Wanamitandao walikuwa na hisia tofauti kuhusu Willy Paul pamoja na mienendo yake. 

Hata hivyo Pozee mara nyingi amepuuzilia mbali madai ya wanamitandao na kuwataka waache kumhukumu.

"Badala ya wanablogu wetu kupost mafanikio yangu na kuhamasisha watu huko nje... wanazingatia upande mbaya tu... tuache upuuzi wote huu tupige muziki mzuri.. namjua Yesu alikataliwa kwao lakini mimi sio Yesu.. tubadilike..." Willy Paul alisema.