"Anjella wamemshika akili ili aondoke" - Harmonize avunja uki,ya, atupa lawama WCB

Msanii huyo aliamua kumwaga radhi kwenye remix ya Champion aliyoshirikishwa na msanii Kontawa.

Muhtasari

• Alisema kuwa kwa sasa wamebaki wawili tu wanaopiga muziki ndani ya lebo yake ambao ni yeye na Ibraah.

Harmonize adhibitisha kuachana na Anjella
Harmonize adhibitisha kuachana na Anjella
Image: YouTube screengrab

Kwa mara ya kwanza Harmonize amevunja kimya kuhusu kuondoka kwa wasanii watatu chini ya miezi miwili kutoka kwa rekodi lebo yake ya Konde Music Worldwide.

Japo hakuzungumza hadharani, msanii huyo alitumia weledi wake katika kutunga mashairi ya kimuziki kulizungumzia hilo ambapo  aliweka wazi kilichotokea kupelekea kuvunjwa kwa mikataba ya wasanii Cheed, Killy na mwanadada Anjella.

Kulingana na Harmonize, Cheed na Killy kuondoka haikuwa kwa ubaya bali ni pengine riziki haikuwa inawakubali wasanii hao na ndio maana wakafikia uamuzi wa kuondoka ili kutafuta chemchemi kwingine.

Alisema kuwa kwa sasa wamebaki wawili tu wanaopiga muziki ndani ya lebo yake ambao ni yeye na Ibraah huku akisema huenda Anjella alitekwa kifikira na tamaa tu na kuondoka.

“Wapiga muziki tumebaki wawili tu, wanangu Cheed na Killy haikuwa riziki. Dadangu Anjella wamemshika akili, waambie Konde Gang ni jeshi la mtu mbili,” Harmonize aliimba.

Pia alipakia vesi hiyo kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo watu walitoa maoni tofauti baadhi wakimkosoa kwa kuwataja watu kwenye mashairi yake na wengine kumsifia kwa ukakamavu alio nao katika kuyaingiza majina ya watu na kuiniana vizuri na vina vya kishairi.

“Tatizo mwanetu umepewa vesi badala uimbe vya maana, wewe unakomalia na kuwataja watu, muziki wa namna hiyo hauwezi kukupeleka kimataifa,” mmoja alisema.

“Wewe Tembo unajua mpaka unakera sana, sasa Asake wa Tandale ndio nani tena?” mwingine alimuuliza kwa utani.

Harmonize adhibitisha kuachana na Anjella
Harmonize adhibitisha kuachana na Anjella
Image: YouTube screengrab