Harmonize akemewa kwa kujifananisha na marehemu Steven Kanumba

"Nikifa leo kila mtu atanizungumzia kama wanavyomzungumzia Kanumba'" alisema Harmonize.

Muhtasari

• Harmonize alitumia ukurasa wake wa Instagram kueleza kujivunia kwake baada ya kukamilisha wimbo 'Champion' 

• Harmonize alimsuta Diamond na kusema kuwa yeye ni Asake wa Tandale huku pia akijipiga  kifua kuwa ametoka nyuma ila amefanikiwa zaidi kuliko mameneja wake akina Babu Tale na Mkubwa Fella.

Harmonize na H-Baba akimsalimu Diamond

Chawa wa mwimbaji wa nyimbo za Bongo Diamond, H-Baba amemzomea Harmonize kwa kujifananisha na marehemu Steven Kanumba.

Harmonize alitumia ukurasa wake wa Instagram kueleza kujivunia kwake baada ya kukamilisha wimbo 'Champion' ambao alishirikishwa na Kontawa.

"Kwa hivyo nikifa leo kila mtu atanizungumzia kama wanavyomzungumzia Kanumba, woow, mniheshimu sasa, nataka kuhisi upendo wenu. Wacha kuficha ukweli, hamna anyeweza kufika kiwango hiki,"  aliandika.

Huku akimjibu bosi huyo wake wa zamani, H-Baba alimwambia kuwa bado hajafika kiwango cha Kanumba ili kujifananisha naye.

Alimwambia mwanamuziki huyo kuwa bado hajulikani vizuri, anajulikana kwenye mtandao wa Instagram tu.

"Kujifananisha na Kanumba ila bado hujafikia alipokuwa mwamba. Wewe ni kama Mwijaku tu hamjapishana. Ili ufike hatua za Kanumba, mpeleke Anjela India kisha ulipe madeni ya watu wanaokudai. Bado wewe ni mdogo wangu, hujafika hatua ya kujulikana. Asanteni, msema kweli naondoka hivyo," alisema.

Harmonize ambaye katika siku za hivi karibuni amekuwa akiendeleza mashambulizi dhidi ya Diamond Platnumz alizidi kumkejeli bosi huyo wake wa zamani akimshtumu kwa kuiba wimbo wa msanii Asake.

Kwenye wimbo 'Champion',  Harmonize alimsuta Diamond na kusema kuwa yeye ni Asake wa Tandale huku pia akijipiga  kifua kuwa ametoka nyuma ila amefanikiwa zaidi kuliko mameneja wake akina Babu Tale na Mkubwa Fella.

“Nimetoboa mbele ya Mkubwa na Tale, kipara (Sallam SK) na Asake wa Tandale. Hizi sio zama za kale, muziki upo huru kama kambi ya kambale,” Harmonize anasikika akiimba kwa ukakamavu na unyama mwingi.