Mapromota walilia hasara baada ya watu 300 tu kutokea kwenye shoo ya Beenie Man

Beenie Man ni msanii mkongwe kutoka Jamaica ambaye anaimba miziki ya Dancehall. Alikuwa na onyesho lake mwishoni mwa wiki iliyopita.

Muhtasari

• Beenie Man alikuwa na onyesho lake katika ukumbi wa Lugogo Cricket Oval siku ya Ijumaa.

Msanii Beenie Man katika tamasha lake Uganda
Msanii Beenie Man katika tamasha lake Uganda
Image: Galaxy TV

Mwishoni mwa wiki jana, msanii mkongwe wa mitindo ya dancehall kutoka Jamaica, Beenie man alikuwa anatumbuiza nchini Uganda lakini tamasha hilo lake limewaacha mapromota katika msongo mkubwa wa mawazo na madeni chungu nzima juu yake, kivipi?

Msanii huyo Anthony Moses Davis a.k.a Beenie Man, alialikwa na mapromota kwa jina Top

Biy Entertainement ambao waliwekeza kwa hali na mali katika shoo yake lakini matokeo yake yakawa ni hasara badala ya faida.

Beenie Man alikuwa na onyesho lake katika ukumbi wa Lugogo Cricket Oval siku ya Ijumaa na shoo hiyo ilivutia umati wa watu wachache zaidi kinyume na matarajio ya mapromota ambao walikuwa wamewekeza wakitegemea kuona umati wa mashabiki wake wengi kutokea.

Kulingana na vyombo vya habari nchini Uganda, watu wapatao 300 tu ndio waliohudhuria shoo hiyo.

“Iliandaliwa na Top Boy Entertainment Records, Beenie Man alitinga nchini Jumatano, Novemba 9, akitumai kuwa angewavutia maelfu ya mashabiki kwenye shoo yake, kutokana na idadi ya nyimbo zilizovuma kwa jina lake na jinsi alivyo na maarufu. Lakini kwa kutamaushwa kwake, washereheshaji walichagua kubaki nyumbani kwa furaha na wengine wakachagua kuhudhuria maonyesho mengine jijini,” kituo kimoja cha redio nchini Uganda kiliripoti.

Mapromota waliopanga tamasha hilo walibaki wakikuna vichwa wasijue pa kuanzia na kudai kwamba wameenda hasara ya karne kwani waliwekeza zaidi ya dola milioni 300 za Kimarekani ila watu walionunua tikiti ni 753 pekee na 300 ndio waliweza kufika katika ukumbi huo.