Meneja wa Diamond amjibu Harmonize kwa kuitukana familia ya WCB

Sallam SK alimjibu Harmonize kwa kumwambia kuwa alishindwa kuendesha lebo na ndio maana wasanii 3 wakaondoka.

Muhtasari

• Awali Harmonize alikuwa amemtaja SK kama kipara kweney vesi ya wimbo wake na Kontawa huku akisema amewapita wote kiriziki.

Sallam SK amjibu Harmonize
Sallam SK amjibu Harmonize
Image: Instagram

Baada ya msanii Harmonize kuachia matamshi ya kumdunisha na kumkejeli meneja wa Diamond, Sallam SK Mendez kwenye wimbo, meneja huyo amejibu mipigo vikali akiita lebo ya Harmonize kuwa himaya ya wagambo.

Kupitia Instagram yake, Mendez ameandika majibu ya kejeli kwa vesi ya Harmonize katika collabo ya remix ya Champion, ngoma ya msanii Kontawa.

Kwahiyo kaua lebo kafungua kundi, wanjiita “Wagambo mtu mbili” au nimeelewa vibaya 😂🤷🏽‍♂️” Sallam SK aliuliza kwa utani kwenye Instagram yake.

Awali tuliripoti kuwa Harmonize kwenye vesi yake katika collabo hiyo na Kontawa aliwaingilia uongozi mzima wa lebo ya WCB huku akiwaita kwa majina ya kuwakebehi.

Alimtaja Sallam SK kama kipara kutokana na mtindo wake wa kunyoa nywele zote muda wote huku akimkejeli Diamond kwa jina Asake wa Tandale kwa mana ya kutonesha kidonda kwenye ile skendo ya kusemekana kuiba wimbo wa msanii huyo wa kimataifa na kuimba kwenye collabo yake na Mbosso.

“Nimetoboa mbele ya Mkubwa na Tale, kipara (Sallam SK) na Asake wa Tandale. Hizi sio zama za kale, muziki upo huru kama kambi ya kambale,” Harmonize aliimba kwa michambo mikali kama kwenye wimbo wa rusha roho.

Baadhi waliotolea maoni yao pale walifurahishwa kujua kuwa kweli ujumbe wa Harmonize uliwafikia walengwa na kusema lengo lake kubwa lilifika hatimaye.

Kumbe huyu Tembo anawanyima usingizi? Mbona mnawaza sana hadi mnanunuwa machawa wamponde lakini wapi? Riziki anatoa Mungu tu. Fanyeni kazi zenu tu mnahofu ya nini?” Salim Nyangatuke alimwambia.

“Kutoboa Mbele Yenu Sio Kazi Ndogo Na Konde Katoboa Lazima Apewe Heshima Yake Yeye Ni CHAMPION Aswaaaa!!” Slim Kazembe alimchamba.

“Kule njaa Kali kumiliki lebo bongo anaemudu ni SIMBA pekee,” Joaqiusam alimuunga mkono.