logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Aliyesema muonekano wa Nameless ni wa kijambazi aomba msamaha

Binafi Nimemfikia Nameless na kumwomba msamaha - alisema.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri16 November 2022 - 09:19

Muhtasari


• Mwanamke huyo alitukanwa na kuhisi kunyanyapaliwa baada ya madai yake ya kukosoa uvaaji wa Nameless kuwachukiza baadhi ya mashabiki kindakindaki wa Nameless.

Aliyemtukana Nameless aomba radhi
Aliyemtukana Nameless aomba radhi

Mwanablogu wa Tiktok ambaye aliwakejeli baadhi ya wasanii wa Kenya waliojitokeza katika onyesho la kwanza la filamu ya kimataifa, Black Panther, ‘Wakanda Forever’ hatimaye amezungumza baada ya kusimangwa vikali na sehemu ya Wakenya.

Mwanadada huyo ambaye ndio mwanzo anaanza safari yake ya kukuza maudhui kwenye mitandao ya kijamii alijipata katika jungu la matusi ya kila rangi baada ya kukejeli muonekano wa msanii mkongwe wa Kenya Nameless akisema kwamba alikuwa anaonekana kama jambazi.

Baada ya video hiyo kuonekana, Wakenya wengi walimjia juu na kumpa mzomo ambao sasa anahisi kabisa wengine walichukua fursa hiyo kumnyanyapaa kutokana na weusi wake na pia sura yake ikiwemo muonekano.

Licha ya hayo, amekubali kuyaogea aliyoyafulia na kuweka wazi kuwa amemfikia Nameless na kuomba samahani kwa matamshi ya kuita muonekano wake kuwa wa kijambazi.

“Binafi Nimemfikia Nameless na kumwomba msamaha na kumwambia kama alichukua kosa kwenye ukaguzi wangu, samahani sana. Pia, nataka kusema hivi nimeona maoni yenu yote na mengi yanahusu ngozi yangu jinsi nilivyo giza na jinsi ngozi nyeusi ilivyo mbaya na jinsi ngozi yangu inavyochukiza watu hamwezi kutumia dakika moja kunitazama,” alisema kwenye video ya Tiktok.

Mwanamke huyo alitukanwa na kuhisi kunyanyapaliwa baada ya madai yake ya kukosoa uvaaji wa Nameless kuwachukiza baadhi ya mashabiki kindakindaki wa Nameless.

“Nameless binafsi unafanana na watu hawa wanaoibia watu kwa sababu ningekuona mimi binafsi ningekimbia maana ni unaonekana majambazi yenye silaha,” alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved