Mbosso afichua sababu ya kuahirishwa kwa ziara yake ya Marekani

Alisema kuwa anaomba radhi kwa mashabiki na mapromota waliokuwa wakimsubiri kumuona.

Muhtasari
  • Aliongeza kuwa tarehe mpya zitatangazwa mara tu atakapopata kibali kutoka kwa daktari wake
  • Aliwahakikishia mashabiki wake kuwa ziara hiyo itafanyika
Msanii Mbosso katika mahojiano ya refresh
Mbosso Msanii Mbosso katika mahojiano ya refresh
Image: Wasafi Media (Youtube screengrab)

Mwanamuziki wa bongo fleva kutoka Tanzania Mbosso amefichua kuwa haendelei vyema kiafya.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagrm  alisema kuwa Daktari amempendekeza asisafiri au kukaa ndani ya ndege kwa zaidi ya saa 8.

Mbosso alitakiwa kwenda kutumbuiza mashabiki wake Marekani.

Alisema kuwa anaomba radhi kwa mashabiki na mapromota waliokuwa wakimsubiri kumuona.

Aliongeza kuwa tarehe mpya zitatangazwa mara tu atakapopata kibali kutoka kwa daktari wake.

Aliwahakikishia mashabiki wake kuwa ziara hiyo itafanyika.

"Halo Mashabiki wangu wa USA, kutokana na sababu za Kiafya, Dk alipendekeza nisisafiri au kukaa ndani ya ndege kwa zaidi ya saa 8

Hii imekuja saa moja wakati ambapo natakiwa kuanza ziara yangu ya Marekani kutoka kwa wikendi ya kutoa shukrani

Natoa pole kwa Mashabiki wangu wote, Mapromota na wote waliokuwa wakisubiri kuniona kwa wakati huu.Ziara mpya itatangazwa mara tu nitakapopata kibali kutoka kwa daktari wangu. . Ninawahakikishia ziara itafanyika, Asante." Aliandika Mbossso.

Mbosso ni miongoni mwa wasanii wa lebo ya WCB ambao wamekuwa wakivuma siku baada ya nyingine kutokana na bidii ya kazi yao ya usanii.