logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nahisi kinyongo! Diana Marua akiri kumuonea wivu vixen aliyedensi na Bahati kwenye wimbo

Bahati alionekana akishika kiuno cha Aggie kwenye video ya wimbo huo.

image
na Radio Jambo

Habari16 November 2022 - 11:29

Muhtasari


• Alipakia video hiyo kwenye ukurasa wake wa Instagram pia kisha kuandika," Nasikia kiwaruu, lakini nitafanyaje?"

Mkewe mwanamuziki Kevin Kioko almaarufu Bahati, Diana Marua amesema kuwa anahisi wivu kumwona mume wake akiinengua kiuno na mwanadada mwingine kwenye video ya wimbo wake mpya.

Kwenye Instastory zake, Marua alipakia video ya wimbo mpya wa Bahati ambao alimshirikisha Aggie the Dance Queen kama vixen wake.

Katika video hiyo, Bahati na Aggie walionekana wakidensi huku Bahati akimshika kiuno mchezaji densi huyo..

"Uuuuwi nahisi kinyongo!! Huyo ni mume wangu!?," Marua aliandika chini ya wimbo huo.

Pia alipakia video hiyo kwenye ukurasa wake wa Instagram pia kisha kuandika," Nasikia kiwaruu, lakini nitafanyaje?".

Baadhi ya mashabiki wake walimtania kwa kumwambia kwamba hawezi kudensi kama Aggie.

Wengine walimwambia kuwa Bahati ni mume wake, anampenda na hakuna anayeweza kuchukua nafasi yake.

"Dee enda ukasikie vibaya na huko," shiku_mkono1 alisema.

"Ni wakati sasa ujiunge na masomo ya kusakata densi baada ya miezi michache," meivin_kelvin alisema.

"Mayoo Diana,huyo Agiie alivyonama,waah,"chillanypinky alisema.

"Yaani huyu ni bibi ya mtu anadensi hivi na bwana ya mtu,"thee_baby.gal alisema.

Hivi majuzi, video ya Bahati na mkewe Terence creative, Milly Chebby akimrombosea Bahati ilikuwa ikisambaa.

Katika video,  Bahati na Milly Chebby walionekana wakijivinjari mbele ya watazamaji kadhaa waliokuwa nyuma ya camera ambao walisikika wakiwashangalia kwa sauti.

Diana Marua alikuwa miongoni mwa waliokuwa wakishangilia wakati mumewe akishiriki kipindi kizuri na mkewe Terence.

Hata hivyo, wakati ambao video hiyo ilisambaa, Marua alikuwa na ujauzito na hakutoa maoni yake.

Vilevile katika mahojiano ya simu na kituo kimoja cha redio cha hapa nchini, Terence aliweka wazi kuwa hana shida yoyote na mkewe kucheza densi na mwanamume mwingine na kufichua kuwa hata mkewe Bahati, Diana Marua alikuwepo wakati hayo yalifanyika na wote walifurahia kutazama.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved