Passaris atangaza kurudi gym baada ya kutoshiriki mazoezi miaka 2 licha ya kulipia

Kando na kufichua habari hizo za kurejelea mazoezi, Passaris aliwashukuru wote waliompigia kura.

Muhtasari

• Katika video hiyo, pia alionyesha mtindo mpya wa nywele, mbali na nywele ndefu kama za farasi anazojulikana nazo.

Mwakilishi wa kike Nairobi, Esther Pasaris
Mwakilishi wa kike Nairobi, Esther Pasaris
Image: Passaris Esher

Mwakilishi wa Wanawake kaunti ya Nairobi Esther Passaris, 58, alienda TikTok mnamo Novemba 15, 2022, kutangaza kwamba alikuwa amerejea kwenye ukumbi wa mazoezi baada ya kupoteza uanachama aliokuwa akilipa kwa miaka miwili iliyopita na kutohudhuria.

Katika video hiyo, pia alionyesha mtindo mpya wa nywele, mbali na nywele ndefu kama za farasi anazojulikana nazo.

Alisukwa nywele zake kwa kusuka, akieleza kuwa ilikuwa ni hatua ya kuzilinda kutokana na mvua inayonyesha jijini Nairobi.

Alidokeza kuwa kwa miaka kadhaa amekuwa akilipia ada ya uanachama kwenye ukumbi wa kufanya mazoezi lakini hajawahi shiriki mazoezi hayo na kusema kwamba safari hii atahakikisha shilingi 2000 zake za uanachama zinafanya kazi kikamilifu.

“Sawa, kwa hiyo nimeegeshwa kando ya barabara. Je, unapenda vipi nywele zangu? Niliamua kusuka nywele zangu kwa kutarajia mvua. Sawa, niliamka saa 4 asubuhi, na niliamua, unajua nini? Nimekuwa nikilipa usajili (uanachama) kwa Parklands Sports Club kwa miaka miwili, na sijawahi kufanya mazoezi. Leo nimeamua sitapoteza shilingi elfu mbili kila mwezi. Kwa kweli nitaenda kwenye mazoezi. Kwa hivyo nimekuwa kwenye mazoezi, nimefanya mazoezi ya Zumba kwa saa moja- ni wazi nimepata kufanya zoezi kwenye viuno vyangu. Nitafanyia mazoezi hatua zangu na kupakia video hizo siku zijazo,” Pasaris alisema kwenye video hiyo.

Kando na kufichua habari hizo za kurejelea mazoezi, Passaris aliwashukuru wote waliompigia kura na kuahidi kuwa anawafanyia kazi kwa jitihada zote kama ambavyo aliwaahidi wakati wa kampeni.

Passaris alichaguliwa kwa mara ya pili mtawalia kama mwakilishi wa kike Nairobi kupitia tikiti ya chama cha ODM ambapo alimbwaga mpinzani wake wa karibu Millicent Omanga aliyekuwa anawania kupitia tikiti ya UDA.