Tunafurahia kukaa na mtoto wetu bila shinikizo la mitandao-Kabi Wajesus afichua haya

Princess ame amefikisha miezi 8 na bado watu hawajamuona. Amesha anza kutambaa bado watu hawajamuona."

Muhtasari
  • Hii imezua sintofahamu tangu wanandoa hao wa nguvu walipomtambulisha mtoto wao wa kwanza wa kiume kwenye mitandao ya kijamii akiwa na miezi mitano
Kabi na Bintiye wa Miezi sita
Image: INSTAGRAM// KABI WAJESUS

Wanablogu Peter Kabi, almaarufu Kabi WaJesus, na Milly Wambui almaarufu Milly WaJesus wa Familia ya Wajesus wamechukua tahadhari kumweka binti yao kwenye mitandao ya kijamii.

Hii imezua sintofahamu tangu wanandoa hao wa nguvu walipomtambulisha mtoto wao wa kwanza wa kiume kwenye mitandao ya kijamii akiwa na miezi mitano na sasa binti yao ana miezi minane na bado hawajamtambulisha kwenye ulimwengu wa mitandao ya kijamii.

Akiwa kwenye mahojiano na Vincent Mboya kwenye chaneli yake ya YouTube inayoitwa 'Vincent Mboya' Kabi Wajesus alifichua kuwa kwa miaka miwili iliyopita maisha yao kama waundaji wa maudhui yamebadilika kweli.

"Kwa life si hugrow natukigrow kuna vitu vingine huchange. Chochote kilichonifurahisha miaka miwili iliyopita huenda nisiwe na msisimko huo kwa sasa.

Princess ame amefikisha miezi 8 na bado watu hawajamuona. Amesha anza kutambaa bado watu hawajamuona."

Alipoulizwa iwapo wakati wowote watamtambulisha kwa mashabiki wao hivi ndivyo alivyosema,

"Kwa sasa tulipo katika maisha kuonyesha mtoto wetu hajaridhika labda kila siku tutafanya. Tuna mambo mengine mengi tunafanya hio si sehemu ya maudhui. Sasa hivi tunafurahia kukaa na mtoto wetu bila shinikizo la mitandao. Nadhani tunafurahia.

Wakati unakuja na tunajisikia vizuri hakika tutakuwa tukimshirikisha kwa watazamaji wetu."