Hisia mseto, Vera Sidika apakia video jamaa akisinzia nyuma

Vera Sidika alipakia video akiwa klabu ambapo mwanaume aliyekuwa nyuma yake alikuwa anasinzia

Muhtasari

• "Huyo mwanaume anayelala anafahamu kuwa yuko kando ya Vera Sidika?"

• Vera alizungumzia video hiyo na kusema kuwa hakufahamu kuwa mwanaume huyo alikuwa nyuma yake hata alipoipakia.

Vera Sidika
Image: Vera Sidika Instagram

Mwanasosholaiti Vera Sidika amezungumzia video yake aliyopakia akiwa klabu huku jamaa aliyekuwa nyuma yake akisinzia.

Aliwajibu wanamitandao waliokuwa wameshangazwa na video hiyo aliyopakia.

Kwenye Instastory zake, kama kawaida, Vera alipakia video hiyo akiwa kwenye klabu katika harakati zake za kazi.

Mwansosholaiti huyo alikana kuwa hakufahamu kilichokuwa kinaendelea na kusema kwamba huwa hajali kuhusu mambo kama hayo.

Jamaa huyo alikuwa na mvinyo wake kando.

Vera Sidika
Image: Vera Sidika Instastory

"Mna ucheshi sana, nikipakia video huwa najiangalia tu. Sijawahi tilia maanani mambo yanayoendela nyuma. Ni nyinyi ndio mnanifanya nitazame video tena kwa sababu ya maoni yenu. Aki woi," Vera aliandika.

Mashabiki wake walitoa maoni yao katika inbox yake kumfahamisha kilichokuwa kinaendelea kisha Vera kuzipakia tena ila alificha majina yao.

Baadhi ya maoni hayo ni:

"Nini kinachoendelea na huyo mubaba, akalale kama amechoka".

"Huyo mwanaume anayelala anafahamu kuwa yuko kando ya Vera Sidika?"

"Huyo mwanaume nyuma yako anakaribia kukuangukia".

"Vera akiwa na juhudi za kuwa malkia, mwanaume nyuma yake anazimia".

Matukio ya Vera Sidika ya kuenda klabu au kuhudhuria hafla kwenye klabu ni jambo ambalo alitangaza kuwa yeye hulipwa kukaa tu na kuwatumbuiza mashabiki wake.

Vera huzuru vilabu tofauti karibu kila siku kama mmojawapo ya kazi anazofanya.

Mwanasosholaiti huyo ni mama ya mtoto mmoja wa kike, Asia Brown na mpenzi wa mwanamuziki wa Kenya Brown Mauzo.

Wawili hao wamekuwa kwenye ndoa kwa takriban miaka miwili sasa .