logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mimi nataka Chang'aa - Samidoh awatania mashabiki wake

“Unaweza kuwa asali ndio, lakini mimi nataka chang’aa,” Samidoh aliandika.

image
na Radio Jambo

Habari17 November 2022 - 10:32

Muhtasari


• Kwa muda mrefu, Samidoh amekuwa akikosolewa kwa kumsaliti Nderitu na kumpenda Nyamu mpaka kupata watoto wawili naye.

Samidoh, msanii na afande

Msanii wa Mugithi ambaye pia ni afisa wa polisi Samwel Michoki almaarufu Samidoh amewaacha watumizi wa Instagram na maswali mengi kichwani baada ya kudai kwamba yeye anataka kileo cha asili aina ya chang’aa.

Samidoh ambaye yupo Marekani kwa wiki kadhaa sasa kwa ajili ya ziara ya kimuziki aliibua swali hilo baada ya kuachia ujumbe changamano akionekana kulinganisha vitu viwili vyenye ladha kinzani – chungu na tamu.

Vile vile katika huo ujumbe wake, baadhi walihisi una mtu alikuwa anachimba mkwara kwa kumkejeli kuwa hata kama yeye ladha yake ni laini na tamu, huenda kwa upande wake akachagua chachu na chungu.

Kwa wapenzi wa vilevi, watakuambia kuwa pombe aina ya chang’aa ni moja kati ya vinywaji vyewe ladha chachu na kali kiasi kwamab mtu akiibugia mdomoni tu hivi anapomeza utamuona amekunja uso na kutokwa na makunyanzi kama panda la uso wa kizee.

“Unaweza kuwa asali ndio, lakini mimi nataka chang’aa,” Samidoh aliandika.

Baadhi walihisi dongo hili lilikuwa linawalenga wale ambao wamekuwa wakimkosoa kwa kumpenda seneta Karen Nyamu licha ya kuwa na mkewe wa kwanza Edday Nderitu.

Kwa muda mrefu, Samidoh amekuwa akikosolewa kwa kumsaliti Nderitu na kumpenda Nyamu mpaka kupata watoto wawili naye.

Samidoh aliwatumia ujumbe changamano kuwa huenda wao wanamshrutisha kuenda kwa asali ambaye ni mkewe Edday lakini kumbe moyo wake umenata na kunasa kabisa kwenye chang’aa kwa maana ya Karen Nyamu.

Kwa upande wako unaelewaje kauli hii kutoka kwa msanii Samidoh?


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved