logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nahitaji dawa na hii baridi - Jimal Rohosafi alia

“Nahitaji dawa na hii baridi,” Jimal Rohosafi aliandika kwenye video hiyo akikariri.

image
na Radio Jambo

Burudani17 November 2022 - 09:19

Muhtasari


• Jimal kupitia Instagram yake, alipakia klipu ya Tiktok yake akikariri baadhi ya mistari ya wimbo mpya wa msanii Mavokali kwa jina Commando.

Jimal Rohosafi

Mfanyibiashara maarufu wa sekta ya matatu nchini Kenya Jimal Rohosafi ameibuka na mapya na kuteta vikali kuhusu kijibaridi ambacho kinazidi kukumba wakaazi wa jiji kuu la Nairobi wiki hii kufuatia mfululizo wa mvua zisizo na kikomo.

Jimal kupitia Instagram yake, alipakia klipu ya Tiktok yake akikariri baadhi ya mistari ya wimbo mpya wa msanii Mavokali kwa jina Commando.

Katika wimbo huo ambao Jimal alikuwa anakariri, moja ya mistari yake inasema kuwa ana baridi na anahitaji dawa ya kutuliza kijibaridi hicho.

“Nahitaji dawa na hii baridi,” Jimal Rohosafi aliandika kwenye video hiyo akikariri.

Ikumbukwe kwa miezi ya hivi karibuni Jimal ameonekana katika msongo mkubwa wa mawazo na dhana ya kukosa mapenzi hasa baada ya mkewe Amira kumbwaga.

Amira alimbwaga mfanyibiashara huyo katika kile kilitajwa kuwa ni kumletea mwanamke mwingine katika ndoa yake. Mwaka jana Jimal aliingia kimapenzi na mwanafasheni Amber Ray.

Baadae mapenzi yake na Ray yaliporomoka na hapo ndio alijaribu kufanya udhubutu wa kurudi kwa Amira lakini akapata mlango umeshafungwa tayari na hivyo kubaki katika hali ya hangulahu – huku hakuna na kule hakuna!

Hivi majuzi, alijipata katika mikwaruzano mikali na wanamitandao baada ya kuachia matamshi yaliyoonekana kuwalenga wanawake kwa njia iliyofurahisha.

“Wanawake huwatengenezea sheria watu wasiopenda kuwa nao, lakini wanavunja sheria kwa wapenzi wanaotaka kuwa nao. Kwa hivyo ikiwa msichana atakuwekea sheria natumai unajua kwanini,” Rohosafi aliandika.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved