Willy Paul awashauri wanaume katika uhusiano wa kimapenzi

Willy Paul amewashauri wanaume kutowapigania wanawake wanaotaka kusitisha uhusiano.

Muhtasari

• "Wanaume wenzangu, iwapo mwanamke anataka kwenda mwache aende," Pozee alisema.

• Haijafahamika ni nani haswa Pozee anazungumzia au kutaka kumfikishia ujumbe huo.

Willy Paul
Image: Willy Paul Instagram

Mwanamuziki Willy Paul amewapa wanaume ushauri kuhusiana na masuala ya kimapenzi.

Kwenye Instastory zake, Willy Paul aliwashauri wanaume kutowabembeleza  sana wanawake ikiwa wanataka mwanamke anataka kuondoka uhusiano.

"Wanaume wenzangu, iwapo mwanamke anataka kuenda mwache aende. Ni wengi wanaokungoja na kukutaka. Kama wewe ni mwaminifu kwake na bado hakuamini basi mwache aende asubuhi na mapema kabla jua liwake," Pozee aliandika.

Alisema kuwa mwanamke anayetaka kusitisha uhusiano yuko kwenye uhusiano na mtu mwingine kwa hivyo mwanamume amruhusu aondoke.

Alisema kuwa mwanamume hafai kujiweka katika hali ambayo wanawake watafahamu kila jambo na mienendo yake. 

Haijafahamika ni nani haswa Pozee alikuwa akizungumzia na ujumbe huo ulikuwa unalenga nani.

Hata hivyo, baadhi ya mashabiki wake wanahisi kuwa staa huyo huenda anasaka tu kiki akijiandaa kuachilia kibao kipya.

Hivi majuzi alitangaza kuwa atawaunfollow baadhi ya watu kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Alisema kuwa atawafuta watu wenye fikira mbaya na raho chafu.

“Kwa hiyo leo nitakuwa nawa-unfollow watu wenye fikira potovu. Ikitokea nimeku-unfollow, tulia tu na ujikusanye na kuendelea na maisha yako…lakini bila mimi,” Willy Paul aliandika huku akimalizia kwa emoji za kucheka.

Hata anapowashauri wanaume hayo, hivi majuzi mwanamuziki huyo alikuwa amefichua kuzama kwenye dimbwi la mahaba na mwanamuziki Jovial.

Wawili hao walikuwa wameweka paruanja mahaba yao mitandaoni na hata kukiri kupendana kwa dhati.

Hata hivyo, 'uhusiano' wao ulidhihirika kuwa ushirikiano katika wimbo walioachia wa 'Lalala' na walikuwa wanatafuta kiki ili kupata wafuasi wa kutazama wimbo huo.

Wawili hao hawajazungumzia kuhusu uhusiano wao baada ya kuachia wimbo huo au kuonyeshana mahaba.