Rapudo aonyesha matukio kwa picha alipokuwa akimvisha pete Amber Ray

Rapudo ameeleza mapenzi yaliyomo baina yake na Amber Ray

Muhtasari

β€’ Kwenye Instagram, Rapudo alipakia picha wakiwa kando ya bahari alipokuwa amemwandalia Amber tafrija ya kimahaba.

Amber Ray na Kennedy Rapudo

Mpenziwe Amber Ray, Kennedy Rapudo amepakia picha za kumbukumbu za siku aliyomchumbia mwansosholaiti huyo.

Kwenye Instagram, alipakia picha wakiwa kando ya bahari alipokuwa amemwandalia Amber tafrija ya kimahaba.

Picha hizo zilionyesha matukio ya kabla, baada na wakati alipokuwa anamchumbia mpenzi wake.

"Lazima tulikuwa wapenzi kwenye maisha mengine, zamani, kwa jinsi tulivyosikilizana kwa haraka mpaka ukawa mchumba wangu. Hii ni kwa ajili ya upendo na urafiki wetu," aliambatanisha picha hizo na ujumbe.

Amber Ray alimjibu kwenye chapisho hilo na kusema jinsi siku hiyo kwa kweli ni ya kukumbukwa.

"Ulikuwa umependeza sana," Rapudo alimwambia.

Wengi walizidi kuwatumia jumbe za kuwaonyesha upendo huku wakiwatakia mema kwa hatua hiyo yao.

"Kosa pesa uchekwe πŸ˜‚πŸ˜‚. Utajua soulmates ni jina tu lisilo na maana... Hata hivyo , mnakaa vizuri pamoja," bundikamencudavid alisema.

"Wapenzi wangu wapendwa wamerudiwa tena❀️❀️ sina mengi ya kusema ni sherehe kubwa sana, asanteni sana," winihj alisema

"Uzuri ya wajaluowanakupenda na roho yao yote hata ukiwa na udhaifu," yvonnebonavy aliandika.

Ninapenda tu furaha iliyo kwenye uso wake, nyinyi wawili mnafaana sana. Hongeraa πŸŽ‰ πŸ‘ Nitazidi kuwapigia wengine makofi hadi zamu yangu ifike πŸ™πŸΌ,"chem.tai alisema.

Amber Ray alivishwa pete ya uchumba na mpenzi wake Kennedy Rapudo wakiwa nchini Dubai.

Rapudo alimpeleka Amber nchini Mauritius ili kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kabla ya kumpeleka Dubai ambapo alimposa Amber.

Mchumba huyo wa Amber Ray alimwandalia tafrija ya kimahaba iliyokuwa na mishumaa kando ya bahari.