(+screenshot) Shakilla afichua Andrew Kibe akijaribu kumtongoza

Katika mazungumzo hayo, Kibe anamuuliza kama amevalia mwanandani jambo ambalo linamkera Shakilla na kuamua kumtumbua.

Muhtasari

• Alimzomea na kusema kwamba mwanablogu huyo ndiye amekuwa akimzungumzia vibaya kwenye podcast zake YouTube.

Shakilla amtumbua Kibe akijaribu kumtongoza
Shakilla amtumbua Kibe akijaribu kumtongoza
Image: Instagram

Mwanasosholaiti mweney utata wingi Shakilla amerudi na umzo kubwa, safari hii akimmwagia mwanablogu wa YouTube, Andrew Kibe maji baridi kwenye upara wa kichwa chake.

Shakila alipakia picha ya mazungumzo yake na Kibe kwenye moja ya DM zake Instagram. Kwenye maongezi hayo, Shakilla alianza kwa kumtaja Kibe kweney moja ya Instastories zake kabla ya Kibe kujibu.

Mazungumzo yao hayakuenda mbali kwani mwanablogu huyo mwenye utata na mazoea ya kuwakejeli na kuwadunisha wanasosholaiti wengi nchini alianza kumtuoia mistari huku akitaka kujua kama alikuwa bila mwanandani.

Shakilla alionekana kuchukizwa na swali hilo na hakusita kumuuliza alikuwa na maana gani kutaka kujua iwapo alikuwa amevali mwanandani au la.

Alimzomea na kusema kwamba mwanablogu huyo ndiye amekuwa akimzungumzia vibaya kwenye podcast zake YouTube lakini hapo alikuwa anaingia kwenye faragha yake kufanya udhubutu wa kumtongoza.

“Nyinyi wote ni wadoeaji. Huyu ni yule jamaa mmoja ambaye anashinda akizungumza mabaya juu yangu lakini leo hii ameingia kwenye DM yangu akinitongoza,” Shakilla aliandika.

Kama wengi wanavyomjua Kibe, ni mtu ambaye ana chuki kubwa dhidi ya wanawake ambayo chanzo chake hakuna anayeweza kuelewa.

Sasa inasubiriwa kuona kama mwanablogu huyo ataingia kwenye YouTube yake na kulitakasa jina lake kutokana na tope hili ambapo Shakilla amelirusha kwenye shati lake jeupe au atanywea na kujifanya hajaona na wala kusikia kile kinachoendelea kuzua gumzo pevu mitandaoni kumhusu na Shakilla.