Nitapambana jino na ukucha na yeyote wa kumsema vibaya mwanangu - Tanasha Donna

“NJ anafanya mambo ya ajabu na kawaida huwa ni chaguo kwangu kutomuonyesha sana kwenye mitandao ya kijamii" - Donna.

Muhtasari

• Ninapenda kumlinda mwanangu kutokana na hilo ili nisionyeshe sana yeye ni chaguo. - Donna.

Donna na mwanawe Naseeb Jr
Donna na mwanawe Naseeb Jr
Image: Instagram//TanashaDonna

Kwa mara ya kwanza mwanamuziki Tanasha Donna amefichua ni kwa nini anapenda sana kumweka mtoto wake Naseeb Juniro mbali na mitikasi yake ya mitandaoni.

Akizungumza kwenye Instagram Live Ijumaa, alibainisha wazi kwamba anamukinga mtoto wake kutokana na watu wenye husda na macho mabaya ambao alisema mtu yeyote awe Muislam au Mkristu anajua kuwa watu kama hao wapo.

Alisema kuwa katika umri aliokuwa nao hakuna mtu anaweza kumbadilisha fikira zake kuwa kuna watu wenye macho mabaya ambayo yanaweza kuleta amdhara katika maisha ya mtu pindi wanapoona maendeleo yako katika mitandao ya kijamii.

“NJ anafanya mambo ya ajabu na kawaida huwa ni chaguo kwangu kutomuonyesha sana kwenye mitandao ya kijamii. Wale ambao ni Waislamu wanaelewa kuwa jicho baya ni la kweli. Ninaamini kabisa kuna watu wenye macho na ndimi mbaya. Mtu yeyote aliyefanikiwa, awepo Mwislamu au Mkristo, awe hamamini Mungu, anaweza kukuambia uende kimya, usimwambie mtu yeyote hatua yako inayofuata kama ataiamini au la. Nadhani hilo peke yake linajieleza,” Tanasha Donna alieleza.

Mama huyo wa mtoto mmoja waliyepata na msanii nguli kutoka Tanzania, Diamond Platnumz alizidi kutoa tahadhari kwamba kinyume na watu wengine wanaosema hawana muda, yeye ana muda kwa mtu yeyote atakayefanya udhubutu wa kumkejeli mtoto wake kwenye mitandao ya kijamii. Alisema muda wa kumpa block mara moja upo tena kwa wingi tu na wala hatosita kuchukua hatua hiyo.

“Ninapenda kumlinda mwanangu kutokana na hilo ili nisionyeshe sana yeye ni chaguo. Wacha niweke wazi kabisa mtu yeyote anayejaribu kumkejeli mwanangu, nitakuzuia mara moja, na sijali nina wakati,” Donna alifoka.