Abel Mutua amwonyesha mkewe mapenzi siku yake ya kuzaliwa

Abel Mutua alimwandikia mke wake ujumbe wa kimahaba

Muhtasari

• "Heri ya kuzaliwa mpenzi wangu na mama ya mtoto wangu! Nakutakia kila kitu ambacho unatamani maishani. Kando na Idris Elba, huyo wachana naye. Nakupenda mpenzi wangu," Mutua aliandika.

• Judy amesherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kutembelea shule ya msingi ya Kumpa Holy Primary School huko Kajiado.

Abel Mutua na Judy Nyawira
Image: Judy Nyawira Instagram

Muigizaji ambaye pia ni mwekekezi wa filamu, Abel Mutua amemwandikia mke wake Judy Nyawira ujumbe wa mahaba akiadhimisha siku ya kuzaliwa.

Kwenye Instagram, muigizaji huyo alimwonyesha mkewe upendo na kuweka picha yake ambayo aliambatanisha na ujumbe mtamu.

"Heri ya kuzaliwa mpenzi wangu na mama ya mtoto wangu! Nakutakia kila kitu ambacho unatamani maishani. Kando na Idris Elba, huyo wachana naye. Nakupenda mpenzi wangu," Mutua aliandika.

Watu wengine mashuhuri walijiunga kumtakia mama huyo heri ya kuzaliwa.

"Heri ya kuzaliwa @judynyawira," kate_actress alisema.

"Heri ya kuzaliwa pacha wa mumbus," aggie_the _dance_queen alisema.

"Heri ya kuzaliwa malkia," millywajesus alisema.

Mashabiki wao pia walimtakia heri ya kuzaliwa.

"Heri ya kuzaliwa Bi Mkurugenzi (Abel Mutua).. Nakuombea maisha marefu.. Ikufurahishe," totohmoreen2021 alisema.

"Scorpio mwenzangu, mimi pia nilisherehekea siku yangu ya kuzaliwa kwa nyumba ya watoto mayatima na kiukweli sijawahi kufurahia siku yangu ya kuzaliwa kama nilivyofurahia," chistinemk alisema.

Judy amesherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kutembelea shule ya msingi ya Kumpa Holy Primary School huko Kajiado.

Alipakia picha zake akiwapakulia watoto uji wakiwa na mume wake.

Jumapili, wapenzi hao walikuwa wanasherehekea kufikisha miaka 14 kwenye ndoa yao.

"Huu mtego hakuna venye angejitoa. Usicheze na mtu ambaye anavaa shati inayofananan na rangi ya basi la chuo kikuu.. huyo ni mtu ambaye ana uwezo wa kuwabeba wasichana wa chuo kikuu. Hata hivyo,kwa ufupi imekuwa miaka 14 sasa, 7 zilizo halali kabisa. Happy anniversary mpenzi wangu!! Kwa miaka mingine," Mutua alimwandikia mke wake ujumbe.