Andrew Kibe haishi kwake! Samidoh amjibu Andrew Kibe baada ya kukosa kumtembelea Marekani

Kibe alimtaja Samidoh akisema ni mnyonge kwa kuwa amewaruhusu wanawake kumpigania kwenye mitandao ya kijamii.

Muhtasari

• Samidoh alisema kuwa Andrew Kibe anaishi kwa Sugar mummy na sio kwa nyumba yake.

Andrew Kibe // Samidoh

Utatanishi umezuka baina ya Andrew Kibe na Samidoh kufuatia safari ya mwanamuziki huyo ya Marekani.

Kibe alidai kuwa mwaka jana, alimwalika Samidoh kwake Marekani na kuahidi kumtembeza na kumwonyesha maeneo tofauti tofauti lakini alipoenda hivi majuzi hakumtafuta.

"Mwaka jana 2021, Samidoh alipokuwa hapa kwa ziara nyingine nilimwomba aje nimuonyeshe miji ya huku siku yake ya mapumziko wikendi . Ili tu kumwonyesha jinsi matajiri wanavyoishi. Nilikuwa nimwalike kwangu," Kibe alisema.

Samidoh alijitetea na kusema kuwa atamtembelea Kibe punde tu atakapopata nyumba yake.

Alidai kuwa Kibe haishi kwake wala peke yake.

"Haha kwani unatakaje? Kwa hiyo, nilikuwa niache kazi yangu kwa sababu kuna mwanaume aliyenikaribisha nyumbani kwa  'sugar mummy' wake?" Samidoh alisema.

Alieleza sababu ya kukosa kumtembelea Kibe.

"Sasa ningekuja aje kwa nyumba ya mama bro? Je, tungeshiriki vipi katika harakati za kunywa kinywaji? Hayo si mambo yanayofanywa na mwanaume kaka. Tulia," Samidoh alisema.

“Sasa wanawake wanamgombania mtandaoni, siwezi kuruhusu wanawake wanipiganie kwenye mitandao ya kijamii, mimi ndiye natakiwa kujua nani wa kuchumbiana naye na lini na si mwanamke," KIbe alisema.

Kibe alimtaja Samidoh kama mwanamume dhaifu kwa kuwa amewaruhusu wanawake kumpigania kwenye mitandao ya kijamii.

"Samidoh wewe ni mnyonge una kipaji lakini nguvu zako zote umeachia wanawake watatu,  wewe unahitaji viboko," alisema.