Diamond asema hata yeye haelewi ni kwa nini kila siku anazidi kupungua uzito wa mwili

Alisema kuwa si yeye tu anazidi kushangaa kutokana na mabadiliko hayo ya mwili wake bali pia hata Watanzania wote

Muhtasari

• Mbosso alimtania kuwa kupoteza kwake uzito wa mwili kunamfanya aonekane kama hana miaka 40 kwenda juu.

Diamond azidi kuingiwa na shaka kupoteza uzito wa mwili wake
Diamond azidi kuingiwa na shaka kupoteza uzito wa mwili wake
Image: Instagram

Diamond kwa mara ya kwanza amezunumzia mwonekano wa mwili wake na kusema kuwa hata yeye haelewi ni kwa nini kila siku anazidi kupungua.

Akiandika katika moja ya picha ambazo Mbosso alipakia kwenye ukurasa wake wa Instagram, Diamond alionesha kushangaa kwake kutokana na kuendelea kupunguka kwa mwili wake na kila siku kuonekana kama kitoto.

Alisema kuwa si yeye tu anazidi kushangaa kutokana na mabadiliko hayo ya mwili wake bali pia hata Watanzania wote wamekuwa wakiibua maswali kama hayo.

“Halafu nimekuwa mdogo, kila siku nazidi kuwa mdogodogo. Hilo swala linawachanganya Watanzania wengi,” Diamond aliandika.

Jibu la Mbosso ndio liliwaacha wengi katika gumzo kubwa kwani walionekana kutolielewa.

Kwa kawaida wengi wanamjua Diamond kuwa wa miaka chini ya arobaini lakini kwa jibu la Mbosso alionekana kudokeza kuwa msanii huyo tajiri wa WCB Wasafi ana miaka zaidi ya 40 hivi.

“Kweli kaka kama hauna miaka 40 vile safi Sanaa,” Mbosso aijibu na kuwaacha wengi kweneye mataa.

Kama unatilia shaka kuhusu kupungua kwa uzito wa mwili wa Diamond Platnumz, ingia kweney kurasa za mitandao yake ya kijamii na upate kutathmini.