Jackie Matubia apakia video wakiwa na mumewe kitandaini

Jumapili za uvivu ni za kupumzika kitandani - Jackie Matubia alisema.

Muhtasari

• Jumapili, Novemba 20, 2022, Matubia alishiriki picha akiwa kitandani kwake tulivu na mpenzi wake.

Jackie Matubia na Blessing Lungaho
Jackie Matubia na Blessing Lungaho
Image: Instagram

Familia ya waigiza Blessing Lungaho na Jakcie Matubia wameendeleza kuonesha mapenzi yao nje na ndani ya nyumba yao.

Jumapili, Jackie Matubia alipakia video kwenye instastory yake ikiwaonehsa wakifurahia wakati maalum ndani ya chumba chao cha kulala.

Matubia na Blessing wamekuwa pamoja kwa miaka miwili na walimkaribisha mtoto wao wa kwanza miezi michache iliyopita. Wapenzi huwa wanaremba matukio pamoja na pia kufanya kazi pamoja.

Jumapili, Novemba 20, 2022, Matubia alishiriki picha akiwa kitandani kwake tulivu na mpenzi wake, ambaye alikuwa ametundika macho yake kwenye skrini ya runinga..

"Tafakari @blessinglungaho ni mpenzi wa shoo za ukweli za kimapenzi. Kwa hivyo hapa nalazimika kutazama. Pia Jumapili za uvivu ni za kupumzika kitandani," aliandika picha hiyo.

Wanandoa hao wamekuwa wakitumikia malengo ya wanandoa, na kushiriki safari yao ya mapenzi kwenye akaunti zao za mitandao ya kijamii, kwa burudani ya wengi.

Hivi majuzi, wapenzi hao wawili waliwapasha watumizi wa mitandao wa kukosoa mitindo ya mavazi yao wakati wa onyesho la kwanza la filamu ya Black Panther Wakanda Forever.

“Mumetuingililia the Lung'ahos. Sijui mara nimesahau corset nyumbani, mara tulienda baby shower, watu wlikuwa na komenti za kuchekesha mpaka tukaanza kucheka. Nilijiona nimependeza, pengine sikukidhi matarajio ya watu, samahani. Tutafanya vizuri zaidi. Wakati ujao, tutafanya uchunguzi kwa ajili yenu nyote, mkuje mtupee anabuni zenu, tuwaulize mnataka tuvae nini,” Matubia alisema huku wakitabasamiana.