Bruce Lee alikufa kutokana na kunywa maji mengi, madaktari wasema miaka 50 baada ya kifo chake

Utafiti mpya umesema alikufa kutokana na matatizo ya figo.

Muhtasari

• Nyota huyo wa Martial arts wa Hollywood alikufa akiwa na umri wa miaka 32 mnamo 20 Julai 1973 akiwa Hong Kong.

Gwiji wa Kung fu Bruce Lee huenda alifariki kutokana na kunywa maji mengi.
Gwiji wa Kung fu Bruce Lee huenda alifariki kutokana na kunywa maji mengi.
Image: INSTAGRAM// Bruce Lee

Gwiji wa Kung fu Bruce Lee alisemekana huenda alifariki kutokana na kunywa maji mengi, madaktari wamedai takriban miaka 50 baada ya kuaga dunia.

Nyota huyo wa Martial arts wa Hollywood alikufa akiwa na umri wa miaka 32 mnamo 20 Julai 1973 akiwa Hong Kong.

Uchunguzi wa maiti ya Lee wakati huo ulionyesha alikufa kutokana na uvimbe wa ubongo, ambao madaktari walimlaumu kwa kutumia dawa ya kutuliza maumivu.

Kifo chake kwa njia hiyo kilipata upinzani mwingi na uvumi wengi wakikataa madai hayo ya kifo cha Lee.

Uvumi ulioenea ulisemekana kuwa Lee  huenda aliuawa na majambazi wa Kichina wengine wakasema alipewa sumu na mpenzi wake mwenye wivu, au ni mwathirika wa laana. Pia nadharia nyingine ilisema kuwa alikufa kutokana na joto.

Sasa, watafiti wamepitia ushahidi wa kutawala kwamba Bruce alikufa kwa hyponatraemia.

Tunapendekeza  Bluce Lee alikufa kutokana na figo yake kutoa maji kupita kiasi,' timu ya wataalamu iliandika katika jarida la Clinical Kidney Journal.

Hyponatremia inamaanisha kiwango kikubwa cha sodiamu katika damu ambacho husaidia mwili kuweka kiwako cha maji cha wastani.

Kukosekana kwa usawa wa maji mwilini husababisha seli za mwili kuvimba, pamoja na zile za ubongo.

Utafiti huo unadai Bruce alikuwa na sababu nyingi za hatari kwa hyponatraemia, ikiwa ni pamoja na kwamba alikuwa akinywa kiasi kikubwa cha maji, akitumia bangi ambayo huongeza kiu pamoja na mambo mengine ambayo hupunguza uwezo wa figo kutofanya kazi sawa kama vile matumizi ya dawa ya kulevya na pombe.

Mkewe Linda alifichua kuwa Bruce Lee alikuwa anapenda kunywa vinywaji vilivyokuwa na maji mengi ya karoti na juisi nyingi kabla ya kifo chake.