Ni 'boyfriend' wangu! Zuchu aweka wazi uhusiano wake na Diamond

Kwenye video, Zuchu alifichua kuwa anampenda sana Diamond

Muhtasari

• Kwenye video ya TikTok, akiwa na rafiki yake, Zuchu aliulizwa ikiwa Diamond ni mpenzi wake.

• "Ndio, huyo ni 'boyfriend' wangu," Zuchu alisema.

ZUCHU NA DIAMOND PLATNUMZ
Image: WASAFI/INSTAGRAM

Mwanamuziki wa Tanzania, Zuchu ameweka wazi kuwa boss wake wa lebo ya WCB, Diamond Pltanumz ni mpenzi wake.

Kwenye video ya TikTok, akiwa na rafiki yake, Zuchu aliulizwa ikiwa Diamond ni mpenzi wake.

"Ndiye huyu?" Rafiki yake aliuliza huku akimwonyesha mwanamuziki huyo picha ya Diamond.

Zuchu alitazama picha hiyo kabla ya kumjibu kisha kukubali kuwa kweli ndiye mpenzi wake.

"Ndio, huyo ni 'boyfriend' wangu," Zuchu alisema.

Rafiki yake alimwonyesha Zuchu kuwa anafurahia mapenzi hayo yake huku akimpongeza kwa kupata mtu.

"Eish, bora una furaha Chummy, umeridhika kwei? Una furaha?" aliuliza.

"Nimezama kwenye dimbwi la mapenzi," Zucu alifafanua.

Diamond na Zuchu, kwa muda mrefu sasa wamekisiwa kuwa wapenzi ila hawajaweka wazi iwapo ni kweli wako kwenye mahusiano.

Hata hivyo, wamekuwa wakiwatania wanamitandao na mashabiki wao kuwa wanapendana ila kiukweli hawajazungumzia suala hilo.

Mwezi uliopita, Diamond hata hivyo kwa mara nyingine aliweka wazi kuwa uhusiano wake na Zuchu ni wa kikazi tu.

Diamond alikana wazi uhusiano wa kimapenzi na mtunzi huyo wa kibao 'Sukari' na kusisitiza kuwa ni msanii wake tu.

Alilazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya mmoja wa mameneja wake, Hamisi Shaban Taletale almaarufu Babu Tale, kumpa shinikizo kubwa  la kumuoa binti huyo wa gwiji wa muziki wa taarab, Khadija Kopa.

"Fanya basi uoe unanichelewesha ujue," Tale alimwambia bosi huyo wa WCB chini ya video aliyopakia kwenye Instagram ikimuonyesha Zuchu akimkabidhi mkufu ghali wa dhahabu kama zawadi ya siku ya kuzaliwa.