Otile Brown afurahia kukutana na wanandoa anaowakubali

Wanandoa Tileh Pacbro na Martina Glez licha ya kutofautiana kwa rangi ya ngozi, walioana na tayari wana mtoto mmoja wa kiume.

Muhtasari

• “Nilikutana na wanandoa wangu pendwa, wataje,” Otile Brown aliandika kwenye rundo la picha Instagram yake.

• Wapenzi hao wawili, Mkenya na Mhispania walitangaza mwaka jana kumkaribisha mtoto wao wa kwanza.

Otile Brown akiwa na familia ya wacheza densi
Otile Brown akiwa na familia ya wacheza densi
Image: Intagram

Msanii Otile Brown ni mtu mwenye furaha baada ya kukutana na wanandoa ambao aliwataja kuwa wenye wanampa motisha sana kutokana na mitikasi yao katika uoande huo wa ndoa.

Alikutana na wanandoa ambao pia ni wacheza densi Tileh Pacbro na mchumba wake mwenye asili ya uzunguni, Martina

“Nilikutana na wanandoa wangu pendwa, wataje,” Otile Brown aliandika kwenye rundo la picha Instagram yake.

Kwa wale hawajui wachumba hao ni wajasiriamali katika sekta ya kusakata densi za kulipwa ambao wana shule yao ya kufunza jinsi ya kunengua viuno.

Mwaka jana walibarikiwa na mtoto wao wa kwanza pamoja, mtoto wa kiume ambaye walifurahia kutangaza kupitia kurasa za mitandao yao ya kijamii.

“Siwezi kueleza hisia niliyokuwa nayo nilipomshika mvulana wangu mdogo @pacbro.jr kwa mara ya kwanza. Ukweli kwamba @martinaglez_ ndiye mtu ambaye atakuwa karibu nami kila wakati katika safari hii hunipa amani na furaha kubwa, hunifanya nijisikie niko nyumbani bado niko mbali sana na nyumbani, asante mtoto kwa kuwa shujaa wangu. Karibu duniani mwanangu!” aliandika Pacbro.

“6/9/2021. Hakuna kitu kitalinganishwa na hiki ninachokupenda zaidi ya nilivyopenda chochote hapo awali na wewe, @tileh_danceking_pacbro asante kwa zawadi kubwa zaidi,” aliandika mwanadada Martina kwenye Instagram yake wakati huo.

Mwanadada huyo mwenye asili ya Uhispania aliwahi nukuliwa akisema kuwa mwanzoni mwa uchumba wao, alisutwa vikali kuwa alikuwa analenga kumlaghai Pacbro pesa zake na wala hakuwa na mapenzi ya kweli naye, jambo ambalo alilikanusha vikali.

Otile Brown anakutana nao wakati ambapo alisema hivi karibuni kuwa hayupo katika uhusiano wowote wa kimapenzi kutokana na kukosa mtu madhubuti wa kukaa naye. Hii ni baada ya uhusiano wake na Mwethiopia Nabayet kuvunjika mapema mwaka huu.