Siku nitafanya collabo na Fally Ipupa, nitakuwa nimefanikiwa kimaisha - Nadia Mukami

Nadia alisema kuwa kwa sasa anajiona wa kawaida sana ila ile siku ya Mungu tu atakapojipata kwenye studio akirekodi wimbo na Fally basi atakuwa ametusua.

Muhtasari

• Siku ambayo nitafanya collabo na Fally Ipupa, nitakuwa nimetusua kimaisha. Kwa sasa bado sana - Nadia Mukami.

Nadia azungumzia collabo ya ndoto zake na Fally Ipupa
Nadia azungumzia collabo ya ndoto zake na Fally Ipupa
Image: Instagram

Malkia wa muziki wa Kenya wa kizazi kipya Nadia Mukami amedhibitisha kuwa ujio wa albamu yake mpya mapema mwaka kesho maandalizi yake yameanza kwa kasi ya 5G.

Akidhibitisha hili kupitia ukurasa wake wa Instagram, Nadia Mukami alisema kuwa kwa sasa inabidi tu amewatesa kwa njaa mashabiki wake kwa muda mchache tu ila mwaka utaanza kwa fujo kubwa kwani albamu yake itasimamisha mawimbi ya soka si tu nchini Kenya bali ukanda wa Afrika Mashariki bila kusaza mataifa ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo na hata Sudan ya Kusini.

Mukami alisema kuwa ndoto yake kubwa ni kuwa na mafanikio makubwa kimuziki na katu hawezi kutebwereka kama hajafanikiwa katika hilo.

Alisema kuwa ile siku atafanikiwa kufanya collabo na staa kutoka DRC Fally Ipupa basi hiyo ndio siku atajihisi kuwa angalau ameifanyia haki safari yake ya muziki na atajipiga kifua kuwa kweli mtoto wa Kenya ametusua.

“Imethibitishwa

“Ninafanyia kazi Albamu yangu! Kitu bora ninachoweza kufanya ni kuwaweka njaa mashabiki wangu kidogo tu! 😁Mapema mwaka ujao, nyote mtapata Albamu! Kutuma Upendo kwa Mashabiki wangu! kaNadians!” Nadia alisema.

“Siku ambayo nitafanya collabo na Fally Ipupa, nitakuwa nimetusua kimaisha. Kwa sasa bado sana… collabo ya ndoto zangu ni Fally,” Nadia aliongeza kwenye instastory yake.

Msanii Fally Ipupani msanii mmoja ambaye kwa sasa anatajwa kuwa mwenye ufuatiliaji mkubwa sana wa kimuziki na ndio maana kila msanii anatamani kufanya collabo naye kutoka ukanda huu.

Ikumbukwe tu kwamab msanii huyo ameshirikiana na msanii mmoja tu kutoka ukanda wa Afrika Mashariki, Diamond Platnumz, wimbo wa ‘Inama’ uliotoka miaka mitatu iliyopita na kuteka mawimbi pakubwa. Wimbo huo ulishikilia usukani kwenye chati za muziki kwa muda kutokana na ubora wake.

Kila la kheri Nadia!