Ni kweli mkiwa kwenye uhusiano muda mrefu mnafanana? Tazama picha za Fred Machokaa na mkewe

Machokaa alipakia picha hizo akimsherehekea mkewe siku ya kuzaliwa kwake.

Muhtasari

• Uendako nitakwenda, utakakokaa mimi pia nitakaa hapo, watu wako watakuwa watu wangu na Mungu wako atakuwa Mungu wangu - Machokaa alisema.

Obachi amsherehekea mkewe siku ya kuzaliwa
Obachi amsherehekea mkewe siku ya kuzaliwa
Image: Facebook

Mtangazaji wa redio mkongwe Fred Obachi Machokaa amemsherehekea mkewe siku ya kuzaliwa kwake kwa kupakia rundo la picha zao tangu walipokuwa vijana wakichumbiana.

Kupitia ukurasa wake wa facebook, Machokaa alimwandikia ujumbe maalumu huku akionekana kunukuu maneno ya Biblia katika kitabu cha Ruth alipokuwa akimhakikishia mama mkwe wake kuwa hangeweza kukaa mbali naye hata kidogo.

“Uendako nitakwenda, utakakokaa mimi pia nitakaa hapo, watu wako watakuwa watu wangu na Mungu wako atakuwa Mungu wangu.....na ndivyo inaendelea!!! Kheri njema ya siku yako ya kuzaliwa mpenzi wangu, nakupenda chembe kwa chembe na unalijua hilo. Safari hii tutasafiri kweli, hivyo Mungu atusaidie,” Obachi alisema.

Fred Obachi Machokaa na mkewe
Fred Obachi Machokaa na mkewe

Mnamo mwaka 2019, Mtangazaji mkongwe wa redio Fred Obachi Machoka na mkewe Sophie walisherehekea miaka 40 ya ndoa katika sherehe ya kupendeza iliyofanyika katika shamba la kifahari huko Isinya, Kaunti ya Kajiado.

Wakirejesha viapo vyao vya harusi, Machoka, ambaye anajivunia kwa jina la kimajazia 'mtu mweusi zaidi katika Afrika ya Weusi', alimfurahisha mkewe walipokuwa wakikaribisha familia na marafiki zao wa karibu kwa hafla yao maalum.

Fred Obachi Machokaa na mkewe
Fred Obachi Machokaa na mkewe

Machokaa alipakia msururu wa picha za enzi hizo wakiwa bado wachumba wachanga ambapo walionekana kudumisha furaha yao ambayo haijaanza leo.

Baadhi ya wanamitandao waliozitazama picha hizo kwa umakini waliwatania kuwa enyewe kukaa pamoja kwa muda mrefu kunawafanya wapenzi kufanana kama mapacha.

“Hivyo ni kweli kwamba mkikaa pamoja kwa muda mrefu mnafanana,” Romanus Owino Ochieng aliandika.

“Uncle Fred umetoka mbali, na ndiyo sabubu Mimi napenda kukusikiliza Mzee! Mungu akuongezee miaka zaidi,” Robert Kweyu Wafula aliandika.

Fred Obachi Machokaa na mkewe
Fred Obachi Machokaa na mkewe
Fred Obachi Machokaa na mkewe
Fred Obachi Machokaa na mkewe
Fred Obachi Machokaa na mkewe
Fred Obachi Machokaa na mkewe