Mapenzi mubashara: Diamond apakia video akimpakata na kumbusu Zuchu

Diamond alikuwa anasherehekea siku ya kuzaliwa kwa Zuchu huku akimwandikia ujumbe wa mapenzi

Muhtasari

• Kwenye Instagram, Diamond alipakia video za kumbukumbu ya mapenzi yake na Zuchu huku akiweka nyimbo za mapenzi.

• "Kumbuka Simba siku zote anakupenda,” Diamond alimwandikia Zuchu.

katika ziara yao ya Ufaransa.
Diamond Platnumza na anayedaiwa kuwa mpenziwe, Zuchu katika ziara yao ya Ufaransa.
Image: INSTAGRAM// ZUCHU

Mwamuziki Diamond amedhibitisha uhusiano wake wa kimapenzi na Zuchu huku akisherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Kwenye Instagram, Diamond alipakia video za kumbukumbu ya mapenzi yake na Zuchu huku akiweka nyimbo za mapenzi.

Mwanamuziki huyo alipakia video wakizurura pamoja, mahali pa kujivinjari, wakibusu na kukumbatiana kwa mahaba.

"Mbona mimi sijui, umenipa nini kidawa, kila unachofanya ni sawa, usiku usingizi sina mpaka ulale wewe,sielewi, ulichonipa mimi sijui. Youll be there for me my baby, ill be there for you my baby, baby wewe ni wangu," alisema kutumia wimbo huo wa Macvoice.

Diamond pia alipakia picha zingine za Zuchu akimtakia heri ya kuzaliwa.

Bosi huyo wa WCB alimwandikia mpenzi wake ujumbe na kumpongeza kwa kuibuka kama msanii mkubwa.

Alimwandikia Zuchu ujumbe wa mahaba kisha kutangaza anavyyompenda mwanamuziki huyo.

“Wiki hii tunaadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa upya kwa msichana mwenye kipawa, mbunifu, upendo, kipaji na mnyenyekevu ambaye Tanzania imebarikiwa na @officialzuchu ...Asante kwa kuendelea kuwafanya Wasafi, Waswahili, Wanawake na Bara zima la Afrika kujivunia,” Diamond aliandika.

Ni faraja kuona ulipoanzia hadi sasa kufikia kuwa miongoni wa Icons kwenye Bara la Africa.. Siku zote kumbuka, kila kazi ina mitihani na changamoto zake....jitahidi kuipokea kila inapokuja na kutafta njia sahihi ya kuishinda, maana tafsiri sahihi ya mtihani ni Kupanda daraja baada ya kufaulu .Mwenyez Mungu akupe baraka na akulinde katika Maisha na safari yako hii ya kuchangia kuonesha Dunia kua WaAfrika tumebarikiwa kipaji kiasi gani… Kumbuka Simba siku zote anakupenda,” Diamond alimaliza kwa hakikisho kuntu.