Msione nacheza Tiktok, kwa akili pia nasoma - Azziad baada ya kuhitimu

Mwanatiktoker huyo alihitimu kutoka chuo anuwai cha KIMC katika kitivo cha uanahabari.

Muhtasari

• Msinione huku mitandaoni nacheza video na huko Tiktok, pia kwa akili tunasoma,” Aziad alisema.

Nasenya ahitimu kutoka KIMC
Nasenya ahitimu kutoka KIMC
Image: Instagram

Mwanatiktoker Azziad Nasenya ni mtu mwenye furaha baada ya kuhitimu kutoka chuo anuwai cha KIMC na shahada ya uanahabari.

Azziad alifichua habari hizo kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii na kuseam kwamba mwisho wa siku amefanikisha ndoto yake licha ya wengi kudhania kuwa hakuwa anafanay kitu cha maana mbali na kuonekana akifanya mitikasi kwenye klipu mitandaoni.

“Elimu ina njia ya kipekee ya kutufanya tuwe na muongozo mzuri wa kufikiria kwa njia sahihi na ndio maana tunafaa kuipata vizuri sababu inatutambulisha jinsi tulivyo. Msinione huku mitandaoni nacheza video na huko Tiktok, pia kwa akili tunasoma,” Aziad alisema kwenye video moja aliyoipakia kwenye instastory yake.

Mwanadada huyo alisisitiza kwamba maombi kwa Mungu ndicho kitu kilichomfanya kumudu mpaka kuhitimu katikati ya kuwa na shughuli nyingi kutoka kuwa na kazi ya redioni asubuhi.

Alisema masomo yake ilimbidi kuyafanya wakati wa ziada jioni baada ya kumaliza kufanya shughuli zingine za siku na aliendelea na mzungumzo huo mpaka kumaliza na kuhitimu.

“Kama si Mungu na kujitolea, kujitutumua usiku na mchana, nisingekuwa hapa. Nilikuwa naamka saa 4 asubuhi kila siku. Ilikuwa ni mapambano,” Nasenya alisema.

Mwanadada huyo alijizolea umaarufu mwaka 2020 wakati wa janga la Korona  baada ya kushiriki katika kufanya challenge ya ngoma ya rapa Femi One akimshirikisha Mejja, Utawezana.