Seneta wa Narok Ledama Olekina amemkashifu Rais William Ruto kuhusu hatua ya kuwaondoa makamishna wanne wanaopinga IEBC.
Katika taarifa yake siku ya Alhamisi, mwanasiasa huyo alisema mchakato wa kuwatimua makamishna hao haukuwa na dhamira kwa vile Ruto sasa ni Rais.
"Je, si jambo la kushangaza kwamba sasa unataka kuwaadhibu makamishna wa IEBC ilhali umepata ushindi? Acha vita hivi visivyo vya lazima. Si thamani yake."
Wanne hao walitofautiana na mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati wakati wa uchaguzi wa urais wa Agosti, na kufichua kutoelewana katika shirika la uchaguzi.
Makamishna hao walikashifu matokeo yaliyompa Ruto ushindi dhidi ya kiongozi wa Azimio One Kenya Raila Odinga.
Ledama alisema huku Ruto akiwa amevuka changamoto iliyotishia urais wake, anafaa kuacha mapigano hayo.
“Mheshimiwa Rais, nilifikiri ulisema tofauti ya walioshinda na walioshindwa katika uchaguzi uliopita ni wale waliomwamini Mungu dhidi ya Wanadamu?,” alisisitiza.
Taarifa yake inajiri saa chache baada ya viongozi wa muungano wa Azimio kuapa kusimama na makamishna hao wa IEBC.
Mr President @WilliamsRuto I thought you said the difference between the winners & loses in the last election was those who believed in God Vs Men? Isn’t ironic that you now want to punish IEBC commissioners yet you got the victory? Stop this unnecessary fights man! Not worth it!
— Sen. Ledama Olekina (@ledamalekina) November 24, 2022