logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Matubia afurahia kupunguza uzito wa mwili miezi 2 baada ya kumeza tembe

Matubia alimeza tembe za kupunguza uzito wa mwili kwa kimombo Allurion Gastric Balloon.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri25 November 2022 - 11:51

Muhtasari


• “Kabla inakutana na baada ya miezi 2 na Allurion Gastric Balloon na mimi ni mtoto mwenye furaha!” Matubia aliandika.

Jackie Matubia

Aliyekuwa mwigizaji nguli wa kipindi cha Zora kilichokamilika katika runinga ya Citizen, Jackie Matubia ni mama mweney furaha baada ya kupitia mchakato wa kupunguza uzito wa mwili wake kwa muda wa miezi miwili na kuona matunda yake jinsi alivyobadilika na kuwa na mshepu wa kutamanisha.

Mama huyo wa watoto wawili alipakia picha mbili alizozishikanisha kwenye Instahram yake – moja ikionesha wakati alikuwa bado hajakumbatia mchakato wa kupunguza uzito na nyingine ikiwa ya sasa, miezi miwili baada ya kukumbatia mchakato huo wa kupunguza uzito wa mwili.

Kinyume na watu wengi ambao huenda mazoezi ya gym kupunguza uzito, Matubia alifichua kuwa yeye hangewezana na bidii ya kila siku kuinua vyuma na ndio maana akazama mkobani na kugharamia mchakato huo wa kupunguza uzito kwa jina Allurion Gastric Balloon.

“Kabla inakutana na baada ya miezi 2 na Allurion Gastric Balloon na mimi ni mtoto mwenye furaha!” Matubia aliandika.

Nchini Kenya watu maarufu wengi wamekuwa wakitaabika na kuongezeka kwa uzito wa miili yao kila uchao pasi na kupata suluhu la kupungua huku wengi wakisema wana uvivu sana wa kushiriki gym kwa ajili ya kufanya mazoezi.

Miezi kadhaa iliyopita mwanahabari Willis Raburu alifichua kwamba alitumia zaidi ya laki 9 kufanya upasuaji wa kupunguza uzito wa mwili wake katika kile alikitaja kuwa hangeweza kumudu kuinua vyumba katika gym.

Hivi majuzi alitangaza kuwa tayari amepunguza uzito wa kilo zaidi ya 30 tangu akumbatie sajari ile.

Kwingineko pia hivi karibuni mwakilishi wa kike kaunti ya Nairobi Esther Passaris alitangaza kurudi gym kwa ajili ya kufanya mazoezi ili kulinda muonekano wake wa kisichana.

Passaris mwenye umri wa miaka 58 alisema kuwa safari hii atahakikisha anajitutumua na kushiriki mazoezi ya gym kinyume na miaka ya nyuma ambayo amekuwa akilipia ada ya uanachama katika gym lakini uvivu unamuingia baada ya siku chache na kusitisha kushiriki mazoezi.

Alisema kuwa ada yake ya uanachama ambayo ni shilingi elfu 2 kwa mwezi itafanya kazi kwani ako na uchu na ari ya kushiriki mazoezi kufa kupona.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved