Mwigizaji Minne Kariuki aomboleza kifo cha baba yake

Mwigizaji na mjasiriamali huyo amekumbwa na majonzi makubwa baada ya kumpoteza babake mpendwa.

Muhtasari
  • Akitumia insta stories Minne Kariuki alichapisha tu picha ya ua jeusi la waridi, na kuisindikiza na nukuu inayosema pumzika kwa amani kwa baba
Muigizaji Minnie Kariuki
Image: Minnie Kariuki/INSTAGRAM

Muigizaji na mjasirimali Minnie Kariuki alifahamika sana kupitia uigizaji wake katika kipindi cha Tabasamu kilichokuwa kinapeperushwa kwenye runinga ya Citizen.

Mwigizaji na mjasiriamali huyo amekumbwa na majonzi makubwa baada ya kumpoteza babake mpendwa.

Alishiriki habari hizo za kusikitisha na wafuasi wake wa instagram Alhamisi usiku.

Akitumia insta stories Minne Kariuki alichapisha tu picha ya ua jeusi la waridi, na kuisindikiza na nukuu inayosema pumzika kwa amani kwa baba.

Minnie hajafichua nini haswa kilichosababisha kifo cha baba yake.

Ingawa haijulikani mengi kuhusu baba wa ukoo,jambo moja tunalojua kwa hakika ni kwamba kabla ya kuaga dunia alikuwa baba mkwe wa  mume  wa mwigizaji huyo Charles Muigai almaarufu Lugz Kenya.

Mapema mwaka huu akiwa kwenye mahojiano mwigizaji huyo alisema kwamba hakutaka kuwa mwigizaji bali alitaka kuwa wakili.

"Nikiwa shule ya upili nilitaka kuwa wakili, lakini nilijijua baada ya kutoka kidato cha nne kwani nilifanya vyema katika uigizaji

Katika uigizaji wa Tabasamu, niliigiza kwa miaka 4, nakumbuka tukipigiwa simu na kuambiwa Tabasamu imekamilika, nililia kwa sababu sikuwa na kazi nyingine

Nilipatwa na msongo wa mawazo kwa miezi 3, niliamua kuanza biashara na nilitamani kazi ya ujenzi," Aliongea Minnie.

Pia muigizaji huyo anaigiza katika kipindi cha Single-ish, na pia aiigiza katika kipindi cha 'My Empress' kilichokuwa kinapeperushwa kwenye runinga ya Maisha Magic East.