Naomba mabinti wetu wavutie wanaume kama Bahati - Diana Marua

Wapenzi hao wanazidisha mapenzi yao mitandaoni wiki kadhaa baada ya wakenya kuwasulubisha kutokana na video ya Marua akizungumzia maisha ya zamani.

Muhtasari

• Bahati alijibu na kusema kuwa ombi kama hilo analikubali ila mwanaume huyo awe na pesa kumliko.

Wapenzi Diana Marua na Bahati
Wapenzi Diana Marua na Bahati
Image: instagram

Mwanablogu wa YouTube ambaye pia ni mwanamuziki wa kutema mistari Diana Marua amemvisha koja la maua mumewe Bahati Kevin Kioko na kusema kuwa angependa sana kama mtoto wao wa kike atavutia mwanaume kama yeye wakati atakapokua mtu mzima wa kutaka kuolewa.

Marua alisema kuwa mumewe Bahati ni chaguo bora kabosa ambalo anaamini ilikuwa bahati kubwa na uamuzi razini kumchagua yeye kuwa mumewe na baba wa watoto wake watatu mpaka sasa.

“Naomba kila siku kuwa mabinti zetu watavutia wanaume wenye moyo na haiba ya mapenzi kama wewe mume wangu Bahati Kenya,” Diana Marua aliandika kwenye Instagram yake huku akipakia picha ya pamoja Bahati akiwa amepiga magoti huku akibusu tumbo la Marua wakati walipokuwa wakitambulisha ujauzito wa mtoto wa tatu kwa wanamitandao.

Kwa upande wake, Bahati alitania kuwa ni kweli mabinti wao wanafaa kujaaliwa mwanaume mwenye mapenzi kama yeye lakini akasema kuwa itakuwa bora zaidi iwapo wanaume wa kuwachumbia mabinti zao watakuwa wenye mihela zaidi kumliko yeye.

“Lakini wanaume hao wawe na pesa kuniliko,” Bahati alijibu.

Wawili hao wanazidisha mapenzi yao mitandaoni wiki kadhaa baada ya Wakenya kuwateketeza kwenye mitandao ya kijamii kutokana na video ya Marua ambayo alifanya miaka miwili iliyopita akieleza kuwa kabla ya kukutana na Bahati, alikuwa mdangaji mwenye wachumba wengi – ambapo kila hitaji la maisha yake lilikuwa na mwanaume maalum wa kulihudumia kwa wakati wake.

Video hiyo iliibuliwa na watu walikuwa wanampa Bahati shinikizo la kumbwaga Diana ila msanii huyo akabaki kwenye msimamo wake wa njia kuu kuwa Diana ndiye mkewem chaguo bora ambalo Mungu alimbariki nalo na atazidi kumpenda bila kujali maisha yake ya awali kabla ndoa.