Nitafunga kurasa za mitandao ya kijamii kisha nitoke mitandaoni-Akothee akiri

Aliendelea na kusema hivi karibuni atafunga kurasa zake zote za mitandao ya kijamii

Muhtasari
  • Yeye ni Miongoni mwa watu mashuhuri wa Kenya ambao wameinuka kutoka kiwango kimoja hadi kingine kutokana na bidii ya kazi yao kwa muda mfupi
Esther Akoth

Ikiwa wewe ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii lazima uwe umekutana na mwanamuziki mashuhuri wa bongo fleva kutoka Kenya Akothe ​​wakati fulani.

Yeye ni Miongoni mwa watu mashuhuri wa Kenya ambao wameinuka kutoka kiwango kimoja hadi kingine kutokana na bidii ya kazi yao kwa muda mfupi.

Siku chache zilizopita alimtambulisha mpenzi wake mpya aliyemtaja kwa jina la Omosh ambaye anaonekana kuanza kubadilisha mwelekeo wa maisha yake.

Kulingana naye, alisema tangu Omosh aingie maishani mwake anahisi kama mke wa nyumbani na mvivu sana kwani anachofikiria ni kulala jioni tu.

Aliendelea na kusema hivi karibuni atafunga kurasa zake zote za mitandao ya kijamii na kutoka kwenye mitandao ya kijamii kwani wana mipango mingi mikubwa ambayo inahitaji umakini wake.

Aliweka wazi kuwa anakuwa mvivu kwani alisema anaenda kulala.

"Tangu Omosh aingie maishani mwangu, ninahisi kama mke wa nyumbani, mimi ni mvivu sana na ninachokiona ni kulala tu mchana.

Hivi karibuni nitafunga kurasa hizi zote Na nitoke kwenye mitandao ya kijamii, tunayo mipango mingi mikubwa inayohitaji umakini. Nimeenda kulala tuonane baadaye,"Akothee aliandika.

Je, unafikiri ni vyema kwa Akothe ​​kuondoka kwenye mitandao ya kijamii?