Pritty Vishy afunguka sababu ya kutemwa na aliyekuwa mpenziwe

Mtumbuizaji huyo alimshauri mpenzi wa sasa wa ex wake kuwa mwaminifu.

Muhtasari

•"Kwa mwanadada anayechumbiana na mpenzi wangu, tafadhali, mtunze vyema. Aliniacha kwa ajili yako," alisema.

•Hivi majuzi aliomba kuwa mke wa mwimbaji wa nyimbo za injili, Daddy Owen .

Pritty Vishy
Image: Pritty Vishy Instagram

Aliyekuwa mpenzi wa Simple Boy, Pritty Vishy amefichua sababu ya kutengana na mpenzi wake.

Kupitia  Instastori zake, mtumbuizaji huyo alimshauri mpenzi wa sasa wa ex wake kuwa mwaminifu.

"Kwa mwanadada anayechumbiana na mpenzi wangu, tafadhali, mtunze vyema. Aliniacha kwa ajili yako," alisema.

Aliambatanisha ujumbe wake na emoji za kuashiria kuvunjika moyo.

Hata hivyo, Vishy hakusema ni mpenzi yupi wake wa zamani haswa ambaye alikuwa akizungumzia.

Kwa kipindi kirefu sasa, malkia huyo mwenye umri wa miaka 21 amekuwa akidokeza kuwa bado yupo ingo baada ya kutengana na aliyedaiwa kuwa mpenzi wake wa hivi majuzi, mwimbaji Madini Classic.

Hivi majuzi aliomba kuwa mke wa mwimbaji wa nyimbo za injili, Daddy Owen ambaye anadaiwa anatafuta mchumba.

Vilevile, alikuwa amedokeza kurudiana na mpenzi wake wa zamani, mwanamuziki Simple Boy.

Katika ujumbe wake, Vishy kwa mikogo ya tausi alisema kwamba hakuna mtu ambaye anaweza kumfanyia Stevo Simple Boy kile ambacho yeye alikuwa anamfanyia .

Aliongeza kuwa daima pengo lake katika maisha ya Simple Boy litabaki kuwa wazi kwani hapajatokea mtu na hapatawahi tokea mtu wa kuliziba pengo lile.

“Mimi nafasi yangu haiwezi kuzibwa kabisa, hakuna mtu anayeweza kufanya kile ambacho nilikuwa nafanya kwa Stevo Simple Boy,” Pritty Vishy alisema kwa madaha.

Aidha alipoulizwa kama huenda hivi karibuni jamii ya wanamitandao ya kijamii watawaona pamoja, Pritty Vishy alidokeza kuwa huenda hivi karibuni wakawa pamoja tena kwa kuwatania watu wawe wapole na kusubiri.

"Ninyi tulieni tu, ngoja mtaona maneno, wekeni bando la kutosha kwenye simu zenu msiwe na wasiwasi,” Vishy alisema.