'Wanaume wanalia kwa sababu ya mapenzi,'Loise Kim awashauri wanawake kuwaelewa wanaume

"Wanaume wanaweza kushindwa kifedha na kujifanya wana kila kitu

Muhtasari
  • Aliendelea na kusema kwamba wanaume pia wana mahitaji ya kihisia, matatizo na bado wanalilia mapenzi na kwa hivyo wanapaswa pia kuzingatiwa
Loise KIm
Image: Instagram

Msanii maarufu wa nyimbo za injili a kikuyu Loise Kim kupitia kwenye ukurasa wake wa Facebook amewashauri wanawake kuwaelewa wanaume wakati mwingine kwani wao pia ni binadamu.

Kulingana naye, alisema kuwa wanaume pia wanaweza kuwa  hawana uwezo wa kifedha na kujifanya kuwa kila kiko sawa kwani wakati mwingine hawana kila kitu ambacho mwanamke anahitaji kutoka kwao.

Aliendelea na kusema kwamba wanaume pia wana mahitaji ya kihisia, matatizo na bado wanalilia mapenzi na kwa hivyo wanapaswa pia kuzingatiwa.

"Wanaume wanaweza kushindwa kifedha na kujifanya wana kila kitu. Wakati mwingine, hana vitu unavyotaka. Wana mahitaji na matatizo ya kihisia. Wanaume bado wanalia kwa ajili ya upendo,"Loise Kim alisema.

Wakenya walikuwa kote katika sehemu ya maoni wakikubaliana naye wakisema alikuwa sahihi kwamba wanaume pia ni binadamu.