Mwigizaji mashuhuri wa Kenya Gloria Songoro almaarufu Jackie leo ameutangazia ulimwengu mzima kwamba anatarajia mtoto.
Mrembo huyo alishiriki habari hizo kubwa kwenye akaunti yake ya Instagram, na hii ilikuwa kupitia chapisho lake jipya zaidi.
Alichapisha klipu fupi ya video alipokuwa amesimama kwenye ufuo wa bahari huku akivalia dera na kofia.
Kilichokuwa wazi kuhusu video hiyo ni kwamba Gloria Songoro alikuwa na ujauzito.
Baada ya kupakia video hiyo mwigizaji huyo alinukuu na kusema;
"Mapigo ya moyo wangu,"Aliandika Gloria.
Mashabiki, na wanamitandao walimtumia jumbe za pongezi na hizi hapa baadhi ya jumbe zao;
celestinegachuhi: 😍😍❤️❤️am so happy for you my boo
nataliegithinji: Congratulations you phenomenal woman.... ❤️❤️❤️❤️❤️❤️hizi baraka ni mob... 😂👏👏proud of you
aggie_the_dance_queen: Aaaw.congratulations twin.You will love this phase😍😍😍
babbiekabae: ❤️❤️❤️❤️❤️Hongera Sana! Am going to be a hot Shosh!!!🔥🔥🔥
jasmine.seventeen: Wooowww 😍❤️❤️❤️ much congratulations babbbbbbyyyyyyy boo .. so happy for you 🙌