Baraka yangu kubwa maishani!Vanessa Mdee amtakia Rotimi heri njema ya kuzaliwa

"Heri ya kuzaliwa🎉 wewe ni mtu mwenye sifa zilizo nadra sana," Mdee alisema

Muhtasari

• Mdee alieleza alisema vile uhusiano wake na Rotimi ni wa karibu na anafurahia kuwa kwenye uhusiano naye.

Vanessa Mdee na Rotimi
Image: Vanessa Mdee Instagram

Mwanamuziki wa Tanzania, Vanessa Mdee amemwandikia mchumba wake Rotimi ujumbe huku akimtakia heri njema siku ya kuzaliwa.

Kwenye ukurasa wake wa Instagram, Mdee aliambatanisha ujumbe huo na video za kumbukumbu akiwa na Rotimi huku wimbo wa 'Everything' wa Mary J. Blije ukiimba.

"Heri ya kuzaliwa🎉  wewe ni mtu mwenye sifa zilizo nadra sana, mara moja maishani, moyo usioweza kufananishwa - Wangu 🥹🙏🏽🤍 . Mungu akubariki, akuhifadhi na akufunike katika jina la YESU. Nakusherehekea siku zote, wewe ndiye baraka kubwa zaidi maishani mwangu na kila siku ni siku ya Ro," Mdee alisema.

Mdee alieleza jinsi uhusiano wake na Rotimi ni wa karibu na anafurahia kuwa kwenye uhusiano huo.

Kwenye wimbo huo wa 'Everything' Mdee alieleza kuwa anapenda kuwa karibu na mchumba wake wakati wote kwani ndiye anayempa furaha wakati anapokuwa na huzuni.

"Nisaidieni kumtakia rafiki yangu wa dhati, Mfalme wangu, Mpenzi wa maisha yangu 😍, Baba ya mtoto wangu, mwendani wangu wa maombi, mwendani wangu wa kibiashara, mpenzi wangu@rotimi💍😍🎉✨," Mdee alisema katika ujumbe wake.

Hivi majuzi, wachumba hao walitangaza kutarajia mtoto wa pili mwaka mmoja baada ya kupata mtoto wao wa kwanza.

Walifichua habari hizo na kutangaza kwamba wanatarajia mtoto wa kike.

" Tunatarajia mtoto wa pili..🙏🏽🎊✨UTUKUFU KWA MUNGU ... ni wa kike 💕," Mdee alisema.

Akizungumza kwenye video iliyochapishwa kwenye ukurasa wake wa Instagram, Rotimi alikiri kwamba kuwa mtoto wa pekee katika familia yao kulimfanya kutaka kuwa na watoto wengi.

Aliongeza kuwa hataki mwanawe awe peke yake.