Esther Musila ni kila kitu kwangu - Guardian Angel amsifia mkewe

Guardian Angel amekuwa akimmiminia Musila mahaba kwenye mtandao

Muhtasari

• "Mke wangu, kila kitu changu," Angel aliandika Instagram.

Esther Musila na Guardian Angel
Image: Guardian Angel Instagram

Mwimbaji wa injili Guardian Angel ameendelea kumnyunyizia mapenzi mkewe Esther Musila kwa njia ya kipekee.

Kwenye Instagram, Guardian Angel alipakia picha yao wakiwa pamoja na kama kawaida yake kuthibitisha mapenzi kwa mkewe kwa maneno.

Mwimbaji huyo alieleza jinsi anavyomthamini mke wake na kusema kwamba, kuwa naye ni zaidi ya kila kitu ambacho ako nacho, anafurahia kuwa naye kama mke wake.

"Mke wangu, kila kitu changu," Angel aliandika Instagram.

"Rafiki yangu wa dhati, mpenzi wangu," Musila alimjibu.

Kwenye picha hiyo, walikuwa wameshikana na kuvaa nguo zinazofanana huku maua yakiwa yamepangwa kando yao.

Mashabiki wao walizidi kuwaonyesha upendo na kuwatakia mema kisha kusifia ndoa yao iliyo na mapenzi mno.

"Watu wangu ninaopenda zaidi, mbarikiwe," tony_tha_deejay alisema.

"Nawapenda sana, Mungu azidi kulinda mapenzi yenu na awatenganishe na adui mwovu shetani,"njeruangie.

Hivi majuzi, mwimbaji huyo alikuwa amesema Musila ni mmoja wa watu ambao hawezi kutafakari maisha bila wao na kudai kuwa ni ‘crush’ wake wa muda wote.

“Kile ambacho Mungu amenifanyia, huyu ndiye crush wangu wa milele,” Guardian Angel aliandika Instagram.

Zaidi ya hayo, mwimbaji huyo alimsifia Musila na kusema kwamba tangu wajuane ameona mafanikio makubwa pamoja na mabadiliko katika maisha yake.

Angel alisema kwamba ameanza kupata mapato ya haiba yake kutokana na muziki wake tangu aanze kuchumbiana na Musila ambaye amembadilisha na kumpa utulivu wa kipiga jeki taaluma yake ya muziki.

Wawili hao wamekuwa kwenye ndoa kwa takribani mwaka mmoja tangu kufunga ndoa yao ya faragha mwezi Januari mwaka huu.

Guardian Angel na Esther Musila walipatana mwaka jana kupitia tafrija iliyowaunganisha.