Sandra Dacha acheza densi na nyanyake, afichua alipoteza watoto wote 8

Alisema kuwa bibio huyo alipowapoteza watoto wote, alidhani maisha yake ndio yamefika mwisho.

Muhtasari

• Dacha alikuwa kijijini akiandaa hafla ya kumbukumbu kwa marehemu wazazi wake.

Sandra Dacha akisakata densi na nyanyake
Sandra Dacha akisakata densi na nyanyake
Image: Instagram

Mwigizaji Sandra Dacha amefichua kuwa nyanya yake aliwahi poteza matumaini ya kupata watoto baada ya kupoteza watoto 8.

Dacha alikuwa na wageni kijijini mwao ambapo alikuwa anasherehekea kumbukumbu ya marehemu wazazi wake ambapo pia akiwa anawasubiri alinengua mauno na nyanya yako huyo katika video ya kupendeza.

Katika video hiyo, Sandra alionekana kutoka kwenye hema alipomkaribia bibi yake mrembo, ambaye aliketi kwenye kiti cha plastiki cha kijani kibichi akiwa amezungukwa na wageni wengine.

Muziki ukiwa umefifishwa kwa mmbali, alisogeza kiuno chake kwa nguvu na kuimba pamoja na wimbo wa kitamaduni.

Hapo ndipo alifnguka kuwa nyanya yake ndiye mtu mmoja anayedumisha furaha yake na kuwa anapomuona na furaha huwa anafarijika sana.

“Hizi zilikuwa nyakati fupi kabla ya wageni wangu kuwasili😹 Nilikuwa chini siku nzima lakini walipopiga simu na kusema walikuwa umbali wa dakika tano…nilichoweza kufanya ni kucheza tu! Kukaribisha watu kijijini ni kazi ngumu naapa🤭 lakini namshukuru MUNGU yote yalikwenda sawa.”

“Wakati huo huo onyesha upendo kwa bibi/mama yangu kwa sababu ndiye mwenye furaha kuliko wote. Anasema alifikiria baada ya kupoteza watoto wake 8, maisha yake yangefikia kikomo lakini anamshukuru Mungu kwa ajili ya wajukuu zake💪🏿 maisha marefu NYADENY!!!” Sandra Dacha alisema.

Alisimama na nyanya yake kutoka vitini na kuanza kucheza densi huku akimfurahia nyanya yake mwenye tabasamu kama lote.