'Uchungu moyoni ni ule ule,'Sandra Dacha awaomboleza wazazi wake

Katika ujumbe huo aliandika jinsi anawakosa wazazi wake, licha ya kutabasamu kila siku.

Muhtasari
  • Mwigizaji huyo alitamani kutumia tu saa moja na wazazi wake.Sandra alifahamika kupitia uigizaji wake kwenye kipindi cha Auntie Boss
Sandra Dacha
Sandra Dacha
Image: Moses Mwangi

Mwigizaji Silprosa almaarufu Sandra Dacha amewaacha mashabiki na wanamitandao wakimtumia jumbe za pole baada ya kuwaomboleza wazazi wake.

Katika ukurasa wake wa facebook, alichapisha picha akiwa amesimama kando ya makaburi ya wazazi wake na kuandika maandishi marefu yenye kugusa moyo.

Katika ujumbe huo aliandika jinsi anawakosa wazazi wake, licha ya kutabasamu kila siku.

Mwigizaji huyo alitamani kutumia tu saa moja na wazazi wake.Sandra alifahamika kupitia uigizaji wake kwenye kipindi cha Auntie Boss.

Alisema,

"Wakati fulani natamani ungekuwa hapa ili niweze kukuambia ni kiasi gani ninakuhitaji ... naficha machozi yangu ninapotaja jina lako lakini UCHUNGU moyoni mwangu bado ni ule ule... ingawa ninatabasamu na kuonekana bila kujali lakini hakuna anawakukosa kama mimi.Je, ninachagua kuamka kila siku na kuhuzunika?HAPANA!Ninaamka kila siku na najua sehemu yangu haipo.

Ikiwa ningeweza kutoa matakwa moja na nisiwe na lingine, ingekuwa kuwa na saa moja na kuitumia pamoja nawe,"Aliandika Sandra.