Watoto wenu wanafanya shughuli gani likizo hii ndefu? - Jemutai auliza

Alipakia picha akiwa na binti wake ambaye watu walizua utani kuwa anamfanana wengine wakisema ni chapa ya Professor Hamo.

Muhtasari

• Jemutai na Professor Hamo wamekuwa wakishirikiana katika malezi ya wanao baada ya kuvurutana hadi vipimo vya DNA.

Mchekeshaji Jemutai na wanawe
Mchekeshaji Jemutai na wanawe
Image: Instagram

Mchekeshaji wa Churchill, Jemutai kwa mara ya kwanza amepakia picha yake pamoja na mtoto wake, picha ambayo wanamitandao wameifurahia kuiona kutokana na tabasamu kubwa ambalo wawili hao wameliweka.

Jemutai aliuliza wafuasi wake na mashabiki kutaka kujua ni nini wanafanya na watoto wao nyumbani, haswa msimu huu ambao watoto wapo nyumbani kwa likizo ndefu kupisha mitihani ya kitaifa na sherehe za krismas.

“Habari za asubuhi, Je! watoto wako wanafanya shughuli gani likizo hii????” Jemutai aliuliza kwenye picha hiyo.

Wanamitandao walijaa kwenye picha hiyo wengine wakilijibu swali lake huku wengine wakizua utani wa jinsi mtoto huyo alikuwa analandama na mchekeshaji Professor Hamo ambaye ni mzazi mwenza wa Jemutai.

Wengine walisema kuwa kukaa na watoto nyumbani katika hii likizo ndefu yenye siku takribani 60 kutoka sasa ni kibarua kigumu sana huku baadhi pia wakisema ni muda mwafaka wa kujaribu kukaa na watoto kwani masomo yalikuwa kama mbio za masafa marefu basi na muda wa kupumzika.

Kucheza tu na kupumzika. Tangu covid iishe masomo yalikuwa mbio za masafa marefu bila muda wa kupumzika,” mmoja alisema.

“Shilingi kwa ya pili ya prof Hamo,” mwingine alisema.

Jemutai na Professor Hamo wamekuwa wakishirikiana katika malezi ya wanao baada ya kuvurutana hadi vipimo vya DNA wakati ilidaiwa Hamo alikataa kutoa matunzo kwa wanawe kuwa si wake.

Katika sakata hilo lililotokea miaka miwili iliyopita, DNA ilidhibitisha kuwa watoto ni wa Hamo na akaamua kuchukua jukumu la kushirikiana na mamake kuwalea japo skendo nzima ilimharibia pakubwa mpaka kupoteza kazi katika kituo kimoja cha redio humu nchini.