Zari ampongeza mpenzi wake Shakib Cham kwa kununua gari jipya

Kando na kununua gari jipya, Shakib pia alikuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Muhtasari

• “Heri ya siku ya kuzaliwa mpenzi wangu na pongezi kwa gari jipya🚘 ❤️🙌. Baraka zaidi babe 💓” Zari alimvisha koja la maua kibenten wake.

Shakib Cham amsherehekea Zari
Shakib Cham amsherehekea Zari
Image: instagram

Kibenten wa mwanamitindo Zari Hassan, Shakib Cham Jumatatu alikuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Shakib, ambaye ni raia wa Uganda, mpenzi wa Zari alipakia picha akiwa ameketi juu ya gari jipya kabisa la manjano aina ya Jeep huku akijisherehekea kwa kuona mzunguko mwingine mpya wa maisha yake.

“Siku yako ya Kuzaliwa ibadilishe chuki yote kuwa upendo, kutofaulu kuwa mafanikio, adhabu zote kuwa baraka na vizuizi vyote kuwa fursa. Nakutakia Siku njema ya Kuzaliwa,” Shakib Cham alijiandikia ujumbe huo mwenyewe.

Mwanasosholaiti Zari Hassan hakuachwa nyuma bali alifika kwenye ukurasa huo wa mpenzi wake mdogo na kummwagia sifa huku pia akitambua gari hilo jipya ambalo alimhongera kwa kufanikiwa kulipata.

“Heri ya siku ya kuzaliwa mpenzi wangu na pongezi kwa gari jipya🚘 🙌. Baraka zaidi babe 💓” Zari alimvisha koja la maua kibenten wake.

Japo haikufahamika ni miaka mingapi kijana huyo Shakib Cham, wengi walimsherehekea na pia kumhongera kwa kupata gari jipya huku baadhi wakitumia fursa hiyo kumteketeza Zari na Kijana wake kwqa kuonesha mapenzi yao mitandaoni licha ya umri baina yao kuwa mpana.

Wiki kadhaa zilizopita, Zari alikuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa ambapo watu kadhaa walimsherehekea.

Kipindi hicho, Zari aliweka wazi kero lake dhidi ya wale waliokuwa wanamkosoa kuchumbiana na kijana huyo mdogo huku akisema kuwa katu hawezi kubali watu kumchagulia maisha ambayo angependa kuishi.

Zari na mzazi mwezake Diamond Platnumz wanatarajiwa kujumuika pamoja msimu huu wa krismas kwa ajili ya wanao na kwa mara kadhaa wengi wamekuwa wakiwashauri kurudiana kwani wanaonekana kushibana pamoja.