logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Maoni kinzani, Arap Uria akizawadiwa runinga 32inch baada ya kukutana na Peter Drury

Baadhi walihisi runinga hiyo ni kidogo kwa umaarufu wake na kutaka apewe ya inchi 60.

image
na Radio Jambo

Habari05 December 2022 - 06:20

Muhtasari


Muuzaji mmoja  wa kuuza bidhaa za kielektroniki nchini ilitangaza kumpa zawadi ya runinga ya kidijitali yenye inchi 32 kwa kufanikiwa kukutana na Drury.

Mchekeshaji Arap Uria afurahia kukutana na Peter Drury

Wikendi iliyopita mchekeshaji maarufu kutoka Kenya Arap Uria alifanikisha ndoto ya maisha yake baada ya kukutana na mta ngazaji maarufu wa sok ya kimataifa, Peter Drury.

Uria alikuwa miongoni mwa watu wenye ushawishi wa kimitandaoni kutoka Kenya ambao walipewa ufadhili kutoka makampuni mbalimbali ya ubashiri na michezo ya Kamari, kuenda Qatar kushuhudia mechi za kombe la dunia.

Akiwa nchini Qatar, Uria aliandika bango na kupiga picha nayo akitoa ya moyoni jinsi alivyotaka kukutana na mtangazaji huyo anayeshabikiwa kwa misemo yake ya utani wakati wa matangazo ya soka.

Jim Beglin, mtangazaji mwenza wa Drury alimhakikishia Uria kuwa atamkutanisha na Drury jambo ambalo alifanikisha.

Uria Jumapili alitangaza kurudi nchini baada ya ziara yake Qatar kukamilika na watu mbali mbali wamekuwa wakimsifia kwa ukakamavu wake wa kuhakikisha lengo lake la kukutana na Drury ambaye ni kama kielelezo chako – Uria amekuwa akifanya maigizo ya matangazo ya mpira akiiga sauti ya Drury kwa muda mrefu.

Kampuni moja ya kuuza bidhaa za kielektroniki nchini ilitangaza kumpa zawadi ya runinga ya kidijitali yenye inchi 32.

Zawadi hii iliibua maoni kinzani katika mtandao wa Facebook ambapo watu waligawanyika kwa makundi, baadhi wakisema ni aibu kwa kampuni hiyo kumpa runinga ndogo kama hiyo licha ya juhudi zake kubwa huku wengine wakiishukuru kwa kutambua mchango wa kijana huyo na kumvisha koja la maua akiwa hai.

“Mmoja wa Wateja wetu Arap Uria alikuwa na ndoto ya kukutana na mshauri wake Peter Drury, hatimaye akafanikiwa. Tunamsherehekea na tunatamani kumzawadia TV ya 32" Smart Tv Hd kwa ajili ya kombe hili la Dunia, tafadhali mtag kama unamfahamu. Hongera kaka yangu Arap Uria,” waliandika.

“Kiwango cha chini, 32inch hakika?? Kwa Arap Uria?? Mnaweza kufanya vizuri zaidi ya hapo...ifanye iwe Top Notch 46"” Michael Wafula Apostle alisema.

“Pea yeye 65 inch. 32" ni ndogo sana kwa mtu mashuhuri,” Amos Kipchumba alisema.

Hata hivyo, Uria alishukuru kwa zawadi hiyo na kusema kuwa angeiendea pindi tu atakapotua nchini kutoka Qatar mapema Jumatatu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved