Mwanablogu Nicholas Kioko na mpenziwe watangaza kutarajia mapacha

Tunayo furaha kuwatangazia kuwa tunatarajia mapacha - Kioko.

Muhtasari

• Alipakia picha za uzinduzi wa ujauzito wote wakiwa wamevalia nguo nyeupe kuashiria furaha na amani.

Nicholas Kioko na mpenzi wake
Nicholas Kioko na mpenzi wake
Image: Nicholas kioko,// Instagram

Mwanablogu wa YouTube Nicholas Kioko na mpenzi wake wameweka wazi kuwa wanatarajia watoto wawili mapacha.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kioko alipakia picha maridadi pamoja na kionjo cha video ya jinsi walifichua ujauzito wao na kusema kuwa ni Baraka kuwa na furaha kuwa ni baba mtarajiwa tena wa mapacha.

“Mioyo yetu imejaa🙏 Miale miwili midogo ya jua kutoka kwa Mungu. Tunayo furaha kuwatangazia kuwa tunatarajia mapacha. Tutashiriki safari yetu na nyinyi ....Mungu ni Mwema,” Nicholas Kioko alisema.

Wanandoa hao ambao wanajulikana kwa video zao za kusisimua za YouTube walikuwa wametania habari hizo kwa muda na kusababisha mashabiki kudhani baada ya kutangaza kuwa walikuwa na habari kubwa za kushiriki.

Katika kurasa zao za mitandao ya kijamii wawili hao walichapisha picha ya skrini iliyosomeka, "pendekeza wakati mzuri....ni rasmi."

Chapisho hilo liliambatana na maandishi, "Leo ni siku yetu ya furaha....Je, uko tayari???????"

Familia na mashabiki walimiminika kurasa zao kuwapongeza na kuwatakia kila la kheri.

Kioko ni mmoja wa wanablogu wa YouTube ambao walipata umaarufu mkubwa kutokana na mahojiano yake ambayo anayafanya na watu mashuhuri nchini.

Mashabiki wao walijumuika nao katika kuwatakia kila la kheri katika safari yao wanayotarajia kuanza kama wazazi wapya.

“Hongera sana kinara, hapa uligonga ndipo na Kheri ya Mungu iwatangulie na kuwaongoza katika safari yenu kama walezi,” mmoja aliandika.