logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kwa nini Kambua amenunua pete baada ya kujifungua

Kambua amekuwa na mtindo wa kununua pete baada ya matukio ya kibinafsi maishani mwake

image
na Radio Jambo

Yanayojiri14 December 2022 - 12:35

Muhtasari


• "Hakika @thevavanistore walinisaidia kumkaribisha binti yangu mdogo kwa pete hii nzuri ✨. Lulu iliyoshikiliwa kwa ustadi na bendi ya dhahabu nyeupe," mama huyo aliandika.

Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Kambua amenunua pete ya lulu kwa ajili ya bintiye ambaye alimkaribisha duniani hivi majuzi.

Kwenye Instagram, Kambua alipakia picha ya mkono wake ukiwa umevalishwa pete hiyo kwenye kidole cha uchumba.

"Hakika @thevavanistore walinisaidia kumkaribisha binti yangu mdogo kwa pete hii nzuri ✨. Lulu iliyoshikiliwa kwa ustadi na bendi ya dhahabu nyeupe," mama huyo aliandika.

Alieleza sababu ya kuchagua pete hiyo na marembesho hayo na kueleza yanaashiria nini kwenye maisha yake .

"Lulu huashiria hekima, uke, utulivu…mambo yote ninayomtakia msichana wangu mdogo. Ninapenda pia kwamba inakamilisha pete zangu zingine. Naipenda. Inapendeza sana unapokuwa na sonara ambaye anakupata kweli, na yote unayowakilisha. 🦋," Kambua alisema.

Mwimbaji huyo amekuwa akitumia pete kama ishara ya kumbukumbu ya wapendwa wake na hata hisia zake maishani.

Mwaka uliopita, Kambua alinunua pete kwa ajili ya mwanawe, Malachi aliyeaga siku chache baada ya kuzaliwa.

Mama huyo wa watoto watatu alipakia picha ya pete hiyo, ambayo ni tofauti na ya sasa na kueleza hisia zake.

" Nilichagua morganite kama jiwe la katikati kwa sababu ni la thamani, hiyo inaashiria uponyaji. Tulizingira morganite na almasi, kwa sababu almasi ni za milele ✨ Inaashiria upendo wangu wa milele. Mawe ya kifahari yamewekwa kwenye waridi la dhahabu . 🤍

Nina hisia za huzuni ninapoandika haya. Nitathamini hili milele. Malachi alikuwa hapa na bado anapendwa sana. Asante Yesu kwa kunipa heshima kubwa ya kuwa mama malaika," mwimbaji huyo alisema .

Kambua amekuwa akisherehekea na kumshukuru Mungu kwa kumpa mtoto mwingine baada ya kumpoteza Malachi.

Alitangaza ujauzito wake hivi majuzi na kuandika ujumbe ulioonyesha furaha ya kuwa mama kwa mara nyingine.

Baadaye, alitangaza kuwa alijifungua mtoto wa kike, miezi miwili iliyopita.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved